A: UTANGULIZI
Idara ya maji inahusika na usimamizi wa sera ya maji ya mwaka 2002 na sheria za maji namba 11 na 12 za mwaka 2009 (National Water policy, 2002, The Water supply and sanitation Act , 2009, The water resources management Act, 2009). Idara hii kwa eneo kubwa inahusika na kusimamia utoaji wa huduma ya maji kwa matumizi ya majumbani, na kiasi Fulani matumizi mengineyo kama viwanda, migodi, kilimo na mifugo.
B: VITENGO VYA IDARA
Idara ina vitengo vifuatavyo:
(i) KITENGO CHA MIPANGO NA UJENZI WA MIRADI (planning and construction section)
• Kufanya usanifu wa miradi , kuandaa nyaraka za mradi
• Kusimamia ujenzi/ukarabati wa miradi mbalimbali
• Kutunza takwimu za miradi inayojengwa/karabatiwa
(ii) KITENGO CHA UENDESHAJI NA MATENGENEZO YA MIRADI (Operations and maintenance section)
• Kusimamia uendeshaji wa miradi vijijini na kutunza kumbukumbu za miradi yote, teknolohjia itumikayo, nishati inayotumika n.k.
• Kutoa ushauri wa kiufundi kwa vyombo vya watumiaji maji, ikiwemo upangaji wa bei ya maji
• Kutoa ushauri wa uhifadhi wa kumbukumbu za uendeshaji wa mitambo, na fedha/mali za mradi
(iii) USAJILI WA VYOMBO HURU VYA WATUMIAJI MAJI ( COWSO registration)
• Kuwezesha wananchi kuunda chombo huru cha uendeshaji na usimamizi wa mradi wa maji vijijini (COWSOs)
• Kusajili COWSOs kwa mujibu wa sheria namba 12 ya mwaka 2009
• Kusimamia COWSO kuendeshwa kwa mujibu wa katiba zao
• Kuwajengea uwezo wa mafunzo mbalimbali COWSO kadri ya mabadiliko ya muda na sheria/kanuni
C: MAJUKUMU YA IDARA:
Majukumu ya Idara ya Maji kwa ujumla ni kama ifuatavyo:
i) Kuandaa mpango wa maji na usafi wa mazingira wa Halmashauri na kuutekeleza kwa kipindi maalumu.(Council Water Supply and Sanitation plan)
ii) Kusimamia ujenzi wa miradi ya maji wilayani kwa fedha za Halmashauri za vijiji, Halmashauri ya Wilaya, Serikali kuu, Wahisani mbalimbali kwa mujibu wa viwango vilivyokubaliwa.
iii) Kusimamia uendeshaji wa miradi ya maji kwa kupitia vyombo huru vya watuamiaji maji (COWSOs)
iv) Kusimamia viwango vya maji (water quality) na viwango vya utoaji huduma (service levels) kwa watumiaji maji vinavyotolewa na COWSOs
v) Kusimamia uhifadhi wa vyanzo vya maji mbalimbali vya asili na vilivyojengwa katika Halmashauri,
vi) Kusajili na kutoa leseni kwa COWSOs ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za maji katika Halmashauri
vii) Kuandaa na kuhuisha Kanzidata za hali ya upatikanaji wa maji katika Halmashauri
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.