• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kampeni ya Ugawaji vyandarua bila malipo yazinduliwa Chalinze

Imewekwa: July 10th, 2025



Na John Mlyambate, Chalinze


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya, Mheshimiwa Shaibu Ndemanga, amezindua rasmi kampeni ya uhamasishaji wa ugawaji wa vyandarua kwa kaya bila malipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya wilaya kilichojumuisha wajumbe mbalimbali wa sekta ya afya.


Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mheshimiwa Ndemanga aliwataka wajumbe hao kuhakikisha jamii inahamasishwa ipasavyo ili kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kupata vyandarua hivyo. Alisisitiza kuwa ugonjwa wa malaria bado ni tatizo kubwa katika maeneo mengi, hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuhakikisha wanajikinga kupitia matumizi ya vyandarua.


Wataalam wa afya kutoka Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais – TAMISEMI walitumia kikao hicho kuwasilisha mipango ya serikali katika kudhibiti malaria, ikiwemo kampeni kabambe ya kugawa vyandarua bila malipo kwa kila kaya kulingana na idadi ya watu waliopo.


Dkt. Peter Gitani kutoka Wizara ya Afya, akiwasilisha mada yake, alieleza kuwa malaria bado ni moja ya changamoto kubwa za kiafya nchini Tanzania. Alibainisha kuwa serikali imeweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha kila kaya inapokea vyandarua bora vya kujikinga na mbu waenezao malaria.


Kwa mujibu wa Dkt. Gitani, katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze pekee, serikali inatarajia kugawa vyandarua 198,101 kwa makisio ya awali. Alieleza kuwa kabla ya zoezi la ugawaji kuanza, watendaji wa vijiji watapatiwa mafunzo maalum kuhusu namna bora ya kuandikisha na kugawa vyandarua hivyo kwa ufanisi.


Alisisitiza kuwa ushiriki wa viongozi wa kijiji, watendaji wa kata, pamoja na kamati za afya ni muhimu ili kuhakikisha mchakato huo unakwenda kwa uwazi na mafanikio, huku lengo kuu likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria nchini.


Kampeni hii ya uhamasishaji na ugawaji wa vyandarua inatekelezwa kitaifa lakini kwa sasa imeanza rasmi katika Mkoa wa Pwani, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali kufikia Tanzania isiyo na malaria ifikapo mwaka 2030.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Kampeni ya Ugawaji vyandarua bila malipo yazinduliwa Chalinze

    July 10, 2025
  • Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

    July 09, 2025
  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.