Kikao cha Kamati ya Ushauri wilaya ya Bagamoyo(DCC) kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze chini Uenyekiti wa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi Zainabu Rashid Kawawa kimeridhia kwa kauli moja Halmashauri ya Chalinze ipandishwe hadhi na kuwa Wilaya.
Katika kikao hicho kilichojumuisha wajumbe kutoka Halmashauri zote mbili za Bagamoyo na Chalinze, Wenyeviti wa Halmashauri,wakuu wa Idara, Maafisa Tarafa, Kamati ya Ulinzi na Usalama na wabunge wote wa majimbo ya Chalinze, Bagamoyo na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Subira Mgalu.
Katika Kikao hicho wajumbe walipitisha ajenda na kusisitiza mipaka ya Halmashauri ya Chalinze ndiyo itakayozingatiwa katika kuipandisha hadhi Halmashauri hiyo na kuwa Wilaya
Kwa upande wake Mheshimiwa Subira Mgalu aliwataka wajumbe wenzake kupitisha suala hili pasipo kuchelewa na hakuna sababu ya kuchelewesha kwani mipaka iko wazi na haina mgogoro wowote.
Baada ya mjadala wa muda mrefu Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Bi Zainabu Kawawa aliwahoji wajumbe kwa pamoja kama wanaridhia hoja hiyo kwa pamoja waliitika ndiyooo.
Aidha Mheshimiwa Kawawa katika hotuba yake ya kufunga kikao aliwataka Watumishi kufanya kazi kwa bidii katika kuwatumikia watanzania na kusisitiza ukusanyaji wa Halmashauri katika Halmashauri zote mbili yaani Bagamoyo na Chalinze.
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.