• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

ABBOT FUND kufadhili ujenzi wa jengo la huduma za dharula Hospitali ya Wilaya Chalinze- Msoga

Imewekwa: September 14th, 2021

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe.  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa jitihada zake katika kuleta maendeleo ya afya nchini kwa kuendelea kuiunga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga mahusiano mazuri na ABBOT.

Ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya Makabidhiano ya Nyaraka za ujenzi na eneo la Ujenzi wa Jengo la matibabu ya dharula (EMD) kutoka ufadhili wa ABBOT ya nchini Marekani ambapo ufadhili huo unagharimu kiasi cha TSh bilioni 1.2 za Kitanzania.

Aidha Mhe. Naibu Waziri amemuahidi Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete kuwa atahakikisha Jimbo la Chalinze litapatiwa gari la wagonjwa moja ambapo ni gari hilo ni moja ya magari 150 yatakayonunuliwa na Serikali inayoongozwa na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan.

" Nafurahi sana kuwa hapa leo kwa rafiki yangu wa siku nyingi Mhe. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa jimbo la Chalinze na katika kumuunga mkono ninamuahidi Mhe. Ridhiwani kumpatia gari la wagonjwa moja kati ya magari 150 ya wagonjwa yanayotarajiwa kununuliwa hivi karibuni ". Alisema Mhe. Mollel

Hata hivyo Mhe.Naibu Waziri wa Afya amewapongeza Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ndugu Ramadhan Possi kwa kusimamia vyema fedha zinazotolewa na Serikali  katika kufanya maendeleo ya sekta ya afya  kwa manufaa ya Halmashauri na ya nchi kwa ujumla.

Aidha nae Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameiomba Ofisi ya Naibu Waziri wa Afya wasichelewe kuanza mafunzo kwa wahudumu watakaohudumia kitengo cha Wagonjwa wa dharula ambapo alisema,

" Ili kuondoa adha ya Wahudumu na wafanyakazi wa huduma za matibabu ya dharula ili hali ujenzi wa jengo umekamilika hivyo hakuna budi kuomba mafunzo hayo yaanze mara moja ". Alisema Mhe. Kikwete.

Hata hivyo Mhe. Rais Mstaafu Kikwete alisema ili kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni lazima kuchapa kazi.

Vilevile Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ameishukuru na kuahidi kutoa  ushirikiano kutoka kwa  Taasisi ya ABBOT kwa ufadhili wa jengo la matibabu ya dharula (EMD) katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze

"Tunawashukuru ABBOT kwa ufadhili huu na pia niwaombe Wananchi wenzangu wa  Chalinze kuweza kutoa ushirikiano na kuulinda mradi huu ili tuweze kufanikisha mradi huu na kuhakikisha  unafanikiwa na kuisha vyema ili kuleta maendeleo ya Afya nchini na kwa Halmashauri kwa ujunla" Alisema Mhe. Ridhiwani.

Kwa mujibu wa Mwakilishi kutoka ABBOT amesema mradi huoo utakuwa wa kwanza kwa ngazi ya Wilaya katika Halmashauri ya Chalinze na pia mradi huo utakamilika ndani ya miezi 12 tu na ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 za kitanzania.

Tukio hilo la Makabidhiano limehudhuliwa na  wageni mbalimbali akiwemo Naibu waziri wa afya Mhe. Dkt  Godwin Mollel,Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa pwani Mhe. Abubakari Kunenge, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Abdallah pamoja na wenyeji wao Makamu Mwenyekiti wa Halmashaurin Mh: Msumi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.