• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkuu wa wilaya ya Kibaha afungua mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani Chalinze na Kibaha

Imewekwa: January 15th, 2026


 

Na John Mlyambate

 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Nickson Simon John, amefungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani wa halmashauri mbili za Chalinze na Kibaha yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

 

Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo madiwani wa halmashauri za wilaya za Chalinze na Kibaha kwa kipindi cha siku tatu mfululizo, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mara baada ya kuchaguliwa.

 

Katika mafunzo hayo, madiwani wanapatiwa elimu katika masuala mbalimbali ikiwemo Uongozi na Utawala Bora, Muundo, Majukumu na Madaraka ya Serikali za Mitaa, pamoja na uendeshaji wa vikao na mikutano katika mamlaka za serikali za mitaa.

 

Vilevile, mada nyingine zinazofundishwa ni Mipango, Bajeti na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo, Usimamizi na Udhibiti wa Fedha, Usimamizi wa Watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu, majukumu, haki na stahiki za diwani.

 

Mafunzo hayo pia yanahusisha maadili ya madiwani, usimamizi wa ardhi katika mamlaka za serikali za mitaa pamoja na masuala mtambuka yanayogusa maendeleo ya jamii na ustawi wa wananchi kwa ujumla.

 

Mafunzo yameandaliwa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kwa lengo la kuwajengea uwezo madiwani katika utendaji kazi wao kwa kuzingatia Katiba, sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji wa mamlaka za serikali za mitaa nchini, sambamba na sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya).

 

Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi, Mheshimiwa Nickson Simon John amewaasa madiwani kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika kuwatumikia wananchi, kutumia kauli za kujenga badala ya kubomoa, na kufanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wa serikali za mitaa bila kuunda makundi, akisisitiza kuwa kiongozi bora ni yule anayewaunganisha wananchi na kuimarisha mshikamano katika jamii.

 

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mandera na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze Mheshimiwa Leon Mgweno ameishukuru serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatawawezesha waheshimiwa Madiwani kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kuzingatiwa utawala bora katika maeneo yao ya kufanyia kazi.

 

Naye Diwani wa kata ya Kiwangwa,Mheshimiwa Malota Kwaga amesema mafunzo hayo ya siku tatu yataimarisha ushirikiano miongoni mwa madiwani,kuwasaidia kusimamia sheria ndogo za halmashauri na kuwajengea uwezo kuhusu nafasi yao kama viongozi wa wananchi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkuu wa wilaya ya Kibaha afungua mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani Chalinze na Kibaha

    January 15, 2026
  • Wazazi na Walezi wafurahia Zoezi la upokeaji na Uandikishaji wa Wanafunzi wa awali, Msingi na Sekondari.

    January 13, 2026
  • Wananchi wahamasishwa kujiunga na bima ya afya kwa wote – Chalinze.

    January 06, 2026
  • Baraza la Madiwani lamchagua Mhe. Leon Lucas Mgweno kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze.

    December 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.