• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Chalinze DC yafanya Kikao cha Baraza la Madiwani kwa Robo ya Pili Mwaka wa fedha 2021/2022.

Imewekwa: February 22nd, 2022

Halmashauri ya Wilaya ya  Chalinze hii leo imefanya kikao chake cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo baraza limepokea taarifa za utekelezaji wa kazi katika ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya pili.

Katika kikao hicho cha Baraza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mhe. Hassan Rajabu Mwinyikondo amewashukuru waheshimiwa madiwani na wataalmu pamoja na Taasisi mbalimbali kwa kufanikiwa kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi kwa maendeleo ya Chalinze.

“Kwanza niwashukuru Waheshimiwa madiwani wenzangu kwa kuweza kufanya kikao chetu cha baraza salama na kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa kazi kwa maendeleo ya Chalinze na kubwa zaidi kuzungumzia mambo muhimu yanayoihusu Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze”. Amesema Mhe. Mwinyikondo.

Hata hivyo Mhe.Mwinyikondo ameziomba vyombo vya ulinzi na usalama kuisaidia Halmashauri ya Chalinze kwenye vita ya ukusanyaji wa mapato,

“Tuna mikakakti katika kukusanya mapato ili kufikia malengo tuliyojiwekwea hivyo basi niwaombe vyombo vya ulinzi na usalama waweze kutusaidia katika shuguli za ukusanyaji wa mapato na wale ambao wanafuja mapato yetu waweze kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria ili Halmashauri yetu iweze kusonga mbele.” Ameongeza Mhe.Menyekiti.

Aidha katika kikao hicho cha Baraza Mbunge wa viti maalum Mhe. Subira Mgalu amezipongeza ofisi ya Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze kwa kutoa zawadi kwa walimiu na kamati za shule ambazo zimefanya vizuri katika utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa ya Mpago wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19  kwa wakati na kutoa wito kwa kamati hizo.

“Kwanza nipongeze ofisi ya Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwazawadia walimu na kamati za ujenzi waliofanya vizuri katika utekelezaji wa ujenzi wa madarasa ya Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 na kutokana na hilo natoa wito kwa kamati hizi kuendelea na kusimamia vyema miradi mingine ya mapato ya ndani na ya Kitaifa.” Amesema Mhe. Mgalu.

Vilevile kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Dorice Mwakatobe ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa hatua inazozichukua za kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato katika Halmashauri. 

“Kwaniaba ya Mkuu wetu wa Wilaya Mhe. Zainabu Abdallah niwapongeze Halmashauri ya Chalinze kwa \ukusanyaji wa mapato na zaidi katika jitihada zenu mnazozifanya za kuhakikisha mnaziba mianya ya upotevu wa mapato katika Halmashauri hii.”Amesema Bi. Dorice Mwakatobe.

Kwa Upande wa uwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mwenyekiti wa Chama hicho kwa Wilaya ya Bagamoyo Ndg.Sharifu amempongeza Mwenyekiti  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na  madiwani kwa kuendesha Baraza kwa weredi  kwa kupata wa fikra na mawazo yao juu ya uendeshwaji bora wa Halmashauri ya Chalinze na kuwaasa wataalamu kufanya kazi kwa ufanisi kwa kufuata maelekezo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi,

“Nikupongeze Mhe. Mwenyekiti,Waheshimiwa Madiwani na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuendesha baraza hili kwa weredi na kuona fikra na mawazo ya kila mmoja wenu juu ya kuiendesha kwa mafanikio Halmashauri yetu ya Chalinze na pia kwakuwa chama chetu cha CCM ndio chenye ilani inayotekelezwa basi wataalamu tukafanye kazi kwa weredi  na kuifuata Ilani inataka inavyotuelekeza kwenye masuala ya kimaendeleo.”Amesema Mhe.Sharifu

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.