Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imefanya kikao chake cha baraza maalum la bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo Baraza lapitisha Bilioni 48.09 kwa mwak wa fedha unaoanza na kuweka kipaumbele katika sekta ya afya ,elimu na Miundombinu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe. Hassan Rajabu Mwiinyikondo ameeleza ni ni kwa namna gani bajeti hiyo ya Shilingi Bilioni 48.09 imegusa sekta muhimu na zenye kipaumbele kwa jamii na kuamini zitatatua kero za wananchi wa Halmashauri ya Chalinze ambapo alisema,
“Katika bajeti hii vipaumbele tulivyoviweka vimegusa mpango mkakaki wa Serikali kwasababu mpango mkakati wa Serikali ni kuiwezesha sekta za afya,elimu na miundombinu hivyo basi katika Bajeti hii ya 2022/2023 naamini inakwenda kutatua changamoto zote za wananchi wetu” Alisema Mhe. Mwiyikondo.
Hata hivyo Mhe. Mwinyikondo amelipongeza baraza la Madiwani kwa kupitisha Bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha ujao kwani ni bajeti inayobeba vipaumbele muhimu kwa jamii naTaifa ili kuondoa kero za wananachi na kuwaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya watendaji na madiwani wa Halmashauri ya Chalinze.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ndg. Ramadhan Possi ametoa shukrani kwa Waheshimiwa Madiwani kwa kupitisha bajeti hii ya Bil. 48.09 kwa mwaka wa fedha ujao na kubainisha miradi ya kimaendeleo itakayoanzishwa katika Halmashauri ya Chalinze.
“ Niwashukuru Waheshimiwa Madiwani kwa kupitisha bajeti yetu kwa mwaka unaokuja na katika bajeti hii tumeweka vipaumbele katika Miradi ya maendeleo kwa sekta ya elimu tumetenga bajeti ya Shiling Mil.300 na sekta ya Afya tumetenga fedha Shilingi Milioni 400 kwaajili ya Hospitali ya Wilaya iliyopo. Alisema Ndg. Possi.
Vilevile MkurugenziMtendaji aliongeza kwa kusema kuwa Halmashauri imetenga fedha kwaajili ya miradi ya Kimkakati ikiwa ni pamoja na maegesho ya magari makubwa,ujenzi wa masoko maeneo mbalimbali na kituo cha Mabasi (Chalinze Bus Stand).
“Kama Halmashauri pia tumeweza kutenga bajeti kwa miradi ya kimkakati ikiwa kwanza Chalinze tuna ukosefu wa maegesho ya magari makubwa mpaka kusababisha magari kuzagaa hovyo hivyo basi tumetenga fedha kwaajili ya ujenzi wa maegesho ya magari makubwa lakini pia Halmashauri tumeanzisha soko katika kata ya Bwilingu ambapo tumeanza kwa hatua ya kwanza na kwa bajeti ya mwaka ujao tumelitengea fedha kwa ujenzi wa awamu ya pili na kwa upande wa kata za Lugoba na Msata tumetenga kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa mgawanyo wa Milioni 100 kwa kila Kata na Kubwa zaidi ni Ujenzi wa kituo cha Mabasi (Chalinze Bus Stand) kwawa awamu ya kwanza na kituo hicho kimeanza kufanya kazi na kwa awamu ya pili tunatenga pesa kwaajili ya kuwezesha kituo cha mabasi kiweze kukamilika ipasavyo”. Alisema Ndg. Possi.
Ikumbukwe kuwa Miradi ya kimkakati yote iliyoanza kufanywa na ambayo imepangwa kufanywa inatumia pesa za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.