• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DC Kawawa awataka wawekezaji wa madini ujenzi kulipa kodi kwa mujibu wa sheria

Imewekwa: May 15th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa amefanya warsha na wadau wa madini ujenzi wa halmashauri ya Chalinze katika Ukumbi wa shule ya Sekondari Lugoba leo na kuwataka kuzingatia sheria taratibu na kanuni za ulipaji ushuru na mapato mbalimbali ya halmashauri  na kukemea utoaji rushwa ili kukwepa ulipaji mapato na shuru mbalimbali ambazo zimeainishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na sheria ndogo za halmashauri.    Mkuu wa Wilaya katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyojumuisha wamiliki wa migodi ya madini ujenzi, kamati ya ulinzi na Usalama na wakuu wa idara wa halmashauri ya Chalinze aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuwa waadilifu kwa kuzingatia sheria ya kupambana na kuzuia rushwa namba 11 ya mwaka 2007 na sheria zingine za nchi zinazohusu mapambano dhidi ya rushwa.     Naye Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Bagamoyo Bwana Raymond Katima alitoa mada ya mapambano dhidi ya rushwa kwa washiriki wa warsha na kuwataka kuzingatia sheria za nchi,pia aliweza kutoa taarifa fupi ya uchunguzi wa namna ya ukusanyaji mapato katika halmashauri ya Chalinze kwa upande wa madini ujenzi na kueleza kuwa mapato yanayotokana na madini kokoto hayakusanywi inavyotakiwa kwani kuna ukwepaji kwa namna moja au nyingine kwa wamiliki wa migodi,KatIma alieleza madhara ya rushwa kwa maendeleo ya nchi na kuwaagiza washiriki katika makampuni yao kuendelea kutoa Elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kila mara kwani rushwa ni suala mtambuka ambalo linatakiwa kuzungumziwa kila wakati mahali pa kazi.     Kamanda wa TAKUKURU aliwasilisha changamoto za kiutendaji katika ukusanyaji wa Mapato na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto hizo ili ukusanyaji wa Mapato ya serikali uweze kutekelezwa kwa mujibu wa sheria na kwa ufanisi zaidi.     Mapendekezo yaliyotolewa katika warsha hiyo ni pamoja na kuweka waangalizi watakaokuwa wanashuhudia namna kokoto zinavyotoka kutoka eneo la uzalishaji kwenda kwa watumiaji,waangalizi hao watakuwa kila sehemu patakapokuwa na uzalishaji wa kokoto ili kudhibiti upotevu wa mapato ya halmashauri. Sanjari na hilo washiriki katika warsha hiyo walikiagiza kitengo cha Tehama kuzikagua mara kwa mara mashine za kukusanyia mapato ili zisihujumiwe na kutumika vibaya na watu wasio waadilifu.     Mheshimiwa Kawawa alimalizia hotuba yake kwa kuwataka wamiliki wa makampuni kuwa wazalendo kwa kulipa kodi na shuru mbalimbali kwa wakati pasipo shuruti na kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa kutoa huduma bora kwa wananchi katika halmashauri ya Chalinze.




Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.