• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Chalinze yapokea ugeni kutoka Halmashauri ya Njombe kwa ziara ya Mafunzo

Imewekwa: July 15th, 2022


Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze hii leo imepokea ugeni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ambapo ugeni huo una lengo la kujifuza Ukusanyaji wa Mapato kupitia Ushuru wa madini ya kokoto pamoja na vyanzo vinginevyo.

Ugeni huo umeongozwa na  na Viongozi wa Halmashauri hiyo ya Njombe  ambaye ni Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe Valentino Aidan Hongoli Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Bi, Sharifa Nabalanganya wakiongozana na baadhi ya Madiwani pamoja na wataalam.

Katika ziara hiyo ugeni huo umepata fursa ya kufanya kikao kifupi ambacho kimejumuisha baadhi ya wataalam kutoka Halmashauri zote mbili ambapo Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ndg. John Mlyambate kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji aliwasilisha taarifa hiyo kwa wageni hao kwa lengo la kuifahamu miradi,vyanzo vya mapato pamoja na jinsi ya ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri.

Mara baada ya Uwasilishwaji wa taarifa hiyo,wageni hao wamepata wasaa wa kutembelea vyamzo mbalimbali vya mapato pamoja na baadhi ya miradi iliyojengwa kwa mapato ya ndani ikiwemo makarasha ya kupasulia kokoto,kituo cha mabasi,soko,vituo vya afya pamoja na Miradi ya Serikali kuu ambayo Halmashauri imetia nguvu katika umaliziaji.

Ndipo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Njombe Mhe Hongoli Ameelezea dhamira iliyowafanya kufika katika Halmashauri hii na jinsi gani wamepokea na taarifa za miradi na vyanzo vya mapato na kujionea vyanzo hivyo amabapo amesema

“Tumekuja  kujifunza kwa jinsi gani mnavyoibua  vyanzo vya mbalimbali vya mapato na namna ya kusimamia vyanzo hivyo na kama tulivyoona kwenye taarifa yenu kuwa mna vyanzo vingi vya mapato kwani tumeona tangu kuanza kwa Halmashauri hii mmeanza na ukusanyaji wa mapato wa Tzs Bil.3.8  mpaka kufikia Tzs Bil.10.7 ambapo hii leo tumeona kuwa mapato yatokanayo na madini ya kokoto kwa mujibu wa taarifa mliyotusomea ndio chanzo kikuu kwa hapa Chalinze na pia hayo yamejidhihirisha  mara baada ya kutembelea baadhi ya makarasha ambayo yanatumika kuzalisha madini hayo”. Amesema Mhe Hongoli.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi Sharifa ameishukuru Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa ukarimu walioupata Chalinze na kuahidi wataendelea kujifunza vitu vingi Zaidi hasa katika ukusanyaji wa mapato wa madini ujenzi.

“ Tunashukuru kwa ukarimu wenu mliotuonesha na tumejifunza vya kutosha hapa Chalinze hasa katika kuibua na ukusanyaji wa mapato wa madini ujenzi kwani ndio chanzo chenu kikubwa cha mapato basi nasi ndio chanzo ambacho tumeakianzisha ikiwa mwanzoni kwa Halmashauri yetu tulikuwa tunategemea ukusanyaji wa mapato hasa katika mazao ya misitu hivyo basi tunaahidi kwenda kuyafanyia kazi yale yote tuliyojifunza kwenu”. Mkurugenzi alisema.

Aidha  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe. Hassan Mwinyikondo kwa niaba ya Halmashauri ameuambia ugeni huo kuwa ujio wao hapa Chalinze umefanya nao kujifunza na kupata mawazo chanya juu ya kuendeleza na kuboresha miradi mbalimbali.

Niwashukuru sana wageni wetu kwa kufika hii leo kwani ujio wenu pia umefanya tubadilishane mawazo mbalimbali yalio chanya ambayo itasaidia  kuendeleza Halmashauri zetu kwa kuibua na kuboresha miradi yetu”. Amesema Mhe.Mwinyikondo.

Hata hivyo Mhe.Mwinyikondo aliendelea kusisitiza ushirikiano baina ya Halmashauri zote hizi mbili katika kupeana ushauri na kuweka uzalendo mbele ili kuzipa maendeleo Halmashauri na Taifa kwa ujumla.

Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bi.Salama Ndyetabura ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Njombe kwa ujio wao na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote ya kujenga yalioshauriwa.

“ Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze ninaomba niwashukuru wageni wetu kwa kufika katika Halmashauri yetu na pia tunawaahidi kuyafanyia kazi yale yote tuliyoyapata kutoka kwenu na pia tunawakaribisha Chalinze siku nyingine kwa ajili ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika Halmashauri yetu na eneo letu kwa ujumla kwani pia tuna mradi wa viwanja kwa baei nafuu vilivyopo eneo la Msolwa”. Amesema Bi. Salama.

Aidha Kuja kwa wageni hao ni muendelezo wa kupokea kundi kubwa la wageni kutoka katika Halmashauri na taasisi mbalimbali nchini ambazo zimekuja kujifunza ni kwa jinsi gani Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze inapiga hatua tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2016 mpaka sasa katika suala la kuibua miradi,ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa fedha za Serikali katika miradi mbalimbali.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.