• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na Shirika la STANDING VOICE zaendesha Kliniki kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Imewekwa: July 2nd, 2022

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kupitia Kitesngo cha Ustawai wa jamii wakishirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Standing Voice imeto huduma za kuelimsisha na ugawaji wa vifaa kinga kwa watu wenye ulemavu wa ngozi katika Hospitali ya Msoga iliyopo katika Halmashauri ya Chalinze.

Akizungumza hii leo Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bi. Shukuru Mgao amesema kama serikali wanajitahidi kutafuta wadau wengi Zaidi ili kuwawezesha watu wenye  ulemavu ili nao wawe moja ya kuiunga mkono serikali ambapo hii leo tumeungana na shirika la Standing Voice kwa lengo la kutoa elimu na kutoa vifaa tiba kwa watu wenye ilemavu wa ngozi.

“ Kama serikali na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kupitia Kitengo cha  Ustawi wa jamii tunajitahidi kuunga mkono juhudi za serikali za kuwasaidia watu wenye ulemavu ambapo kwenye hilo tumeungana na Shirika la Standing Voice kwaajili ya kutoa elimu juu ya kujikinga na saratani ya ngozi pamoja na kutoa vifaa kinga kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi”. Amesema Bi.Mgao

Bi. Mgao aliongeza kwa kuwaomba wadau mbalimbali kuendeleza utamaduni na kujitokeza kwa wingi juu ya kuwasaidia watu wenye ulemavu kwani kwa kufanya hivyo wataendeleza na  kuisaidia Serikali juu ya dhamira yake ya kuwasaidia walemavu nchini.

Aidha kwaniaba ya Mwakilishi wa shirika la Standing Voice Bi.Valeria Mambya ameelezea lengo kuu la lililowafanya kufika katika Halmashauri ya Chalinze ili kutoa huduma hiyo.

“ Leo tumefika hapa katika Hospitali ya Msoga kwa lengo la kufanya kliniki ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo tunaungana na timu ya madaktari mbao watatoa elimu, vifaa kinga na kuwapima ngozi na kuwapatia matibabu kwa wale watakaokutwa na viashiria vya saratani na kwa wale waliothirika watapatiwa rufaa na kutibiwa katika Hospitali kubwa za KCMC na Muhimbili na gharama zake zote zitalipwa na shirika letu.” Amesema Bi. Mambya.

Hata hivyo Bi Mambya ameongeza kwa kusema kuwa Kiliniki ya leo imeambatana na kugawa vifaa kinga kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo mwamvuli mmoja kwa kila mtoto mdogo lakini pia kila mmoja atapewa,kofia na mafuta maalumu ya kukinga miale ya jua inayosababisha saratani.

Vilevile Daktari wa ngozi kutoka Kitengo cha ngozi katika Hospitali ya KCMC Dkt. Aidan Mashuhuri ameelezea ni kwa namna gani anawatibu na kuwapa elimu walemavu wa ngozi ambao wamefika katika kliniki hiyo na kuwapa ushauri mbalimbali.

“Kikubwa tunafanya uchunguzi wa ngozi zao ili kuona viashiria vya awali vya saratani na kutoa matibabu kwa kutumia  ( Liquid Nitrogen)  na kwa wale wenye saratani tayari tunapiga picha sehemu iliyoathirika na kujaza kwenye kifaa maalumu cha kuhifadhia data na kumpa rufaa ili aweze kutibiwa katika Hospitali kubwa za KCMC na Muhimbili bila malipo”. Amesema Dkt. Aidan Mashuhuri.

Nae mwakilishi wa kundi hilo lenye ulemevu wa ngozi  Bi.Christina Thobias ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa jitihada inayofanya juu ya kutafuta wadau mbalimbali ambao wanatoa huduma mbalimbali zinazowalenga walemavu.

“ Kwa niaba ya wenzangu ninapenda  kutoa shukrani zangu za dhati kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa kutuletea shirika hili la Standing Voice ambalo hii leo limetupatia elimu mbalimbali hasa inayohusu namna ya kutunza ngozi zetu na pia kutupatia vifaa kinga kama vile kofia na mafuta ya kutunza ngozi zetu dhidi ya mionzi ya jua na tunapenda kusema waendelee na moyo huo”. Amesema  Bi .Christina Thobias.

Kliniki hiyo kwa walemavu wa ngozi inaendeshwa kwa siku moja tu ya Tar 01/07/2022 na pia Shirika hilo limeahidi kurejea katika Halmashauri ya Chalinze mnamo mwezi wa 12 mwaka 2022.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.