• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango yakagua Vyanzo vya Mapato

Imewekwa: August 18th, 2018

Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango imekagua vyanzo vya Mapato katika Halmashauri ya Chalinze kwa kutembelea mgodi wa Kokoto wa  YAATE Investment Co Ltd,na kuona uzalishaji na ubora wa kokoto zinazozalishwa katika mgodi huo. Mgodi huo ni mgodi unaozalisha kokoto zinazotumika kujenga Reli ya kisasa "Standard gauge" kutoka Dar es salaam hadi Morogoro kwa awamu ya kwanza. Mgodi huu ni mgodi unaotoa kokoto bora kwa Afrika Mashariki na Kati,lakini pia Kokoto kwa Chalinze ni chanzo kikuu cha Mapato kinachoiwezesha Halmashauri kutekeleza miradi ya Maendeleo na utoaji huduma za Jamii.

Wajumbe wa Kamati hii wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe.Madaraka Mbode waliishukuru kampuni kwa uzalishaji wa Kokoto bora ambayo imekubalika kimataifa hata kutumika katika ujenzi wa Reli ya kisasa na kusababisha Halmashauri kupata Mapato ya kutosha kutokana na uhitaji mkubwa wa madini hayo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za Jamii Mhe.Malota Kwaga aliwapongeza kampuni ya YAATE kwa kuwa waaminifu katika kulipa Mapato ya Halmashauri na serikali kwa ujumla na kuwasisitiza kutunza takwimu zao za uzalishaji Kokoto kwa uhakiki pindi zinapohitajika na wadau.

Aidha Kamati ya Fedha ilitembelea katika eneo la Ujenzi wa ofisi ya Halmashauri katika mji wa Chalinze na kukagua namna Ujenzi unavyoendelea. Kwa mujibu wa Msimamizi wa Ujenzi wa jengo hilo,Bwana John Chizima alieleza Ujenzi huu upo katika hatua ya kwanza yaani Ujenzi wa Msingi na baada ya hapo hatua ya pili itafuata. Katika Ujenzi huu kuna changamoto zinazopelekea Ujenzi kusuasua ni kukosekana kwa nishati ya umeme kwa ajili ya Kazi ya kuchomelea vyuma na matumizi mengineyo. Katika ukaguzi huo Kamati iliagiza suala la umeme lishughulikiwe na Mhandisi Mshauri kwa kushirikiana na Menejimenti ya Halmashauri ili Ujenzi ueweze kuendelea kwa kasi na umalizike kwa mujibu wa mkataba."Tunaagiza suala la upatikanaji Umeme litafutiwe ufumbuzi haraka iwezekanavyo na shughuli za ujenzi ziendelee."Mbode alisema.

Ujenzi wa Msingi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze katika Mji wa Chalinze ,ukiwa katika hatua za awali.

Wajumbe wa Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango wakipata taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Halmashauri.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.