• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kikwete aipongeza benki ya NMB

Imewekwa: October 7th, 2018

Na. John Mlyambate,Chalinze

Mbunge wa jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete ameipongeza Benki ya Nmb kwa juhudi zao za kutoa misaada kwa jamii ili kutatua changamoto mbalimbali zinazokuwa zikiwakabili wanajamii.

Akitoa pongezi hizo jana, katika kata ya kiwangwa alipokuwa akipokea vifaa tiba mbalimbali  vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Zahanati ya Kiwangwa,Ridhiwani alisema kuwa swali zahanati hiyo ilikuwa na changamoto ya vitanda kwa ajili ya kinamama kuweza kujifungulia lakini kutokana na msaada huo tatizo hilo limebaki kuwa ni historia .

“Naipongeza benki ya Nmb kwa kutambua thamni ya kinamama wa chalinze ingawa katika nchi yetu kuna changamoto nyingi sehemu zingine lakini nyie mmeamua kutuletea msaada huu katika halmashauri yetu ya Chalinze”Alisema Ridhiwani

“Mimi nawatia moyo tu kwa niaba ya wananchi wa Chalinze msichoke kutusaidia kwani mahitaji yetu bado ni mengi ingawa nasi kama serikali tunapambana ili kuhakikisha kinamama wanajifungua bila matatizo ya aina yeyote hivyo ndiyo maana hata vifo vya kinamama wajawazito vinazidi upungua na kubaki kuwa historia”Mbunge alisisitiza.

Aliongeza kuwa awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vitanda kwa ajili ya akinamama kujifungulia katika zahanati hiyo lakini Nmb imewapatia vitanda 10 kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo hivyo amewataka wananchi wa kata hiyo kwa kushirikiana na watumishi wa zahanati hiyo kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo ili viweze kuwasaidia kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze Dkt. Rahim Hangai alisema kuwa kipindi cha nyuma kinamama walikuwa wanapoteza maisha yao wakati wa kujifungua kutokana na changamoto mbalimbali kwa sasa ni wastani wa mama mmoja hupoteza maisha kwa mwaka kati ya  akinamama laki moja wanaojifungua hii ni hatua kubwa sana katika halmashauri yetu ya Chalinze.Alisema.

Aidha Dkt. Hangai alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja kwa muda muafaka kutokana maombi yetu ilikuwa ni kupata vifaa na Nmb wametuletea hivyo vifo vinavyotokana na uzazi itabaki kuwa historia kwa halmashauri ya Chalinze. "Natoa maagizo kwa watumishi wa idara ya afya katika halmashsuri ya chalinze kila mmoja kwa nafasi yake afanye kazi kwa bidii na kwa kuzingatia maadili ya kazi yake ili kuokoa maisha ya mama na mtoto ili Chalinze tumalize tatizo hili kama siyo kupunguza."‎Hangai alisema.

Naye Meneja wa Benki ya Nmb wilaya ya Bagamoyo Bi, Bertha Mungure alisema kuwa benki hiyo imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika jimbo la Chalinze, vyenye thamani ya shilingi ya milioni kumi kwa lengo la kutoa faida wanazozipata kwa jamii ili kuisaidia serikali baadhi ya changamoto zinazokuwa zikiwakabili wananchi.

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa kipindi chote kwani kwa kipindi hiki benki imetenga fedha nyingi za kusaidia katika jamii ili kuweza kulipa fadhila kwa wateja wake.

“Vifaa vilivyotolewa ni vitanda vya kujifungulia 10,vitanda vya kawaida 6,magodoro 10,'delivery kit' 1 na Bm Mashine 6 vyote vikiwa na thamani ya fedha za kitanzania milioni 10”Alisema Meneja huyo.

Aidha amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa ushirikiano na benki hiyo kwa kuwahamasisha wananchi wake kufungua akaunti katika benki ya Nmb na kuachana na tabia ya kukaa na pesa ndani ya nyumba.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.