• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Maandalizi ya Maonyesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yapamba moto

Imewekwa: July 29th, 2025

Na John Mlyambate 


Maandalizi ya maonyesho ya Nanenane katika Kanda ya Mashariki yameingia katika hatua za mwisho, ambapo maonyesho hayo yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 1 Agosti 2025 na kufikia kilele chake tarehe 8 Agosti 2025. Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka yatajumuisha mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam na yatafanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, uliopo katika Manispaa ya Morogoro.


Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, maandalizi kwa ajili ya kushiriki maonyesho hayo yamekamilika kikamilifu. Halmashauri imehakikisha kuwa mazao mbalimbali ya mfano (vipando) na teknolojia mpya zinazohusiana na sekta za kilimo, mifugo na uvuvi zimeandaliwa kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi na wadau mbalimbali watakaotembelea banda la Chalinze.


Aidha, Halmashauri ya Chalinze imesisitiza kuwa lengo la ushiriki wao ni kuhakikisha wananchi wanapata uelewa mpana wa mbinu bora za uzalishaji, usindikaji wa mazao, ufugaji wa kisasa pamoja na uvuvi wenye tija. Kupitia maonyesho haya, wakulima, wafugaji na wavuvi watajifunza njia mpya za kuongeza thamani ya mazao na bidhaa zao ili kuongeza kipato na kukuza uchumi wa kaya.


Vilevile, teknolojia mbalimbali za umwagiliaji, utunzaji wa ardhi na uhifadhi wa mazingira zitatolewa ili kuhakikisha wakulima na wafugaji wanaboresha tija bila kuathiri rasilimali asilia. Banda la Chalinze pia litakuwa na maafisa ugani, wataalam wa mifugo na wataalam wa uvuvi watakaotoa elimu ya moja kwa moja kwa wananchi watakaofika kujionea shughuli hizo.


Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki mwaka huu yanatarajiwa kuvutia wadau wengi kutoka sekta za umma na binafsi. Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea banda lao ili kunufaika na teknolojia, maarifa na mbinu mpya zitakazowasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo endelevu ya uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Maandalizi ya Maonyesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yapamba moto

    July 29, 2025
  • Halmashauri ya wilaya ya Chalinze kujenga kituo cha mafuta kwa mapato ya ndani

    July 16, 2025
  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze Atembelea maonyesho ya 49 ya Saba saba

    July 14, 2025
  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.