• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Maelekezo ya Uchaguzi Serikali za Mitaa yatolewa

Imewekwa: September 24th, 2019


Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya  Chalinze Ndugu Shaban Milao ametoa maelekezo ya Uchaguzi  siku ya Jumatatu(jana) tarehe 23.09.2019 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Chalinze mbele ya Watendaji wa kata, Viongozi wa vyama vya Siasa na Menejimenti kama ilivyoelekezwa kwenye kanuni na  na mwongozo wa Uchaguzi ambapo maelekezo hayo yalilenga  jinsi gani utaratibu wa Uchaguzi utakavyokuwa.

Ndugu Milao ameanza kwa kutangaza  siku ya Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba  kama ilivyobainishwa na kutangazwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Seleman S. Jafo Mwezi Agosti 2019..

‘Natangaza kwa kurudia tangazo la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Seleman S. Jafo kuwa  Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika tarehe 24 Novemba 2019,  vituo vyote vitafunguliwa saa 2 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni, Kupiga kura ni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni na Uchaguzi Utafanyika katika Majengo ya Umma na si ya vyama vya siasa,  pale ambapo hakuna jengo la Umma uandikishaji utafanyika sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atakuwa amekubaliana na Viongozi wa Vyama vya Siasa, mara baada ya upigaji kura vituo hivyo vitabadilika na kuwa vituo vya kuhesabia kura.’’

Vile vile Ndugu Milao aliendelea kwa kuzungumzia suala la sifa za mpiga kura ambazo ni pamoja na awe ni raia wa Tanzania, awe na umri wa miaka 18 au zaidi, awe  ni mkazi wa kijiji au kitongoji au mtaa ambao Uchaguzi unafanyika,awe hana ugonjwa wa akili uliothibitishwa na daktari anayetambulika na Serikali au Bodi ya Utabibu na awe amejiandikisha kupiga kura katika kitongoji, mtaa au kijiji husika.

Pia Msimamizi wa uchaguzi alitangaza tarehe ya kutolewa kwa fomu za wagombea ambapo kuanzia tarehe 29 Oktoba hadi tarehe 4 Novemba, 2019 kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Licha ya hayo  Ndugu.Milao alieleza kuwa kutakuwa na uteuzi wa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ambapo baadhi ya watumishi wa Umma ngazi ya kata watateuliwa na kumsaidia msimamizi wa Uchaguzi na kuwasihi baadhi ya Watendaji wa kata wasiopata nafasi ya kuteuliwa na walioteuliwa waendelee na kusimamia Uchaguzi uende vyema na kwa amani katika maeneo yao.

Ndugu Milao ameongeza kwa kusema..

“Kila Msimamizi Msaidizi atatakiwa kuhakikisha kuwa fomu za wagombea zinakuwepo za kutosha na zitatolewa bila masharti wala malipo ya aina yoyote  na mgombea atakaechukua fomu ya kugombea nafasi ya uongozi atahakisha anarejesha fomu husika ndani ya  muda wa siku saba tangu siku ya kwanza ya utoaji fomu hivyo basi kuanzia tarehe 5 Novemba  majina yote ya wagombea yatabandikwa  ndani ya kata husika na kuanzia tarehe hiyo 5 Novemba 2019 hadi 7 Novemba, 2019 ni siku ya kuweka Pingamizi kwa wagombea na uamuzi wa pingamizi hilo utatolewa kupitia kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kulingana na vithibitisho husika.’’

Aliongeza kwa kusema kama kuna Pingamizi lolote dhidi ya Wapiga kura waliojiandikisha hali ya kuwa si wakazi wa kijiji au kitongoji husika basi pingamizi hilo lifikishwe kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi na kulitolea maamuzi kwa kufuata taratibu husika na uthibitisho dhidi ya pingamizi hilo. Aliendelea kwa kusema ..

‘’ kutakuwa na Kamati ya Rufani itakayo husika na rufaa dhidi ya pingamizi la uteuzi, kamati hiyo itaundwa na wajumbe ambao ni Katibu Tawala wa Wilaya, Watumishi wanne wa Umma kutoka wilaya husika na mtumishi wa Umma mmoja kutoka Ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya.’’

Pia alitangaza rasmi siku ya kampeni za uchaguzi ambazo zitaanza mnamo tarehe  17 Novemba hadi tarehe 23 Novemba, 2019 na kila chama cha siasa kitawasilisha ratiba yake ya kampeni kwa Msimamizi wa Uchaguzi ndani ya muda wa siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni na kupanga vyema ratiba hiyo ili kuwakabidhi Viongozi wa Vyama na Kituo cha polisi Wilaya nakala za ratiba hiyo kwa lengo la  kuondokana na muingiliano wa shughuli za kampeni za vyama mbalimbali.

Hata hivyo Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu Lington Zambi amemalizia kwa Kuwaomba wajumbe wote kuanzia ngazi ya kata mpaka vijiji kushirikiana vyema katika kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndani ya Halmashauri ya Wilaya Chalinze unafanyika kwa amani na kuhakikisha maagizo yote yaliyotolewa yanafanyiwa kazi.

Aliongeza kuwa

‘’Nawakumbusha baadhi ya watendaji watakaochaguliwa kuwa Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wahakikishe wanatoa fomu za kugombea kwa wagombea ambao watawasilisha barua maalumu kutoka kwenye Vyama vyao vya Siasa vinavyowadhamini kugombea nafasi husika.’’AlIsema Bw. Zambi.

Mwisho ndipo uteuzi kwa baadhi ya watendaji wa kata ulifanyika kwa kukabidhiwa barua rasmi na kuwa Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.

Kulingana na maelekezo ya Uchaguzi yaliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi kama ilivyo kwenye Mwongozo wa Uchaguzi ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa umesaidia kuweka wazi mtiririko mzima wa Uchaguzi utakavyokuwa ndani ya Wilaya katika Vijiji, Mitaa na Vitongoji husika.

 

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.