• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkurugenzi Mtendaji Chalinze afungua mafunzo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu

Imewekwa: September 26th, 2025

Na John Mlyambate


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, leo amefungua rasmi mafunzo kwa wajasiriamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waliokidhi vigezo vya kupata mikopo inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo. Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa sheria inayoweka masharti ya kutenga sehemu ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwainua kiuchumi wananchi kutoka makundi maalum.


Mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo walengwa katika masuala ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha na uendeshaji wa biashara. Wawezeshaji kutoka sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya fedha, biashara, kilimo na maendeleo ya jamii wanatarajiwa kutoa mada muhimu zitakazosaidia washiriki kuboresha mbinu zao za kibiashara na kuhakikisha kuwa mikopo watakayopata inaleta tija.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkurugenzi Possi amesisitiza umuhimu wa washiriki kuwa makini wakati wa kupokea mafunzo hayo. Ameeleza kuwa elimu watakayoipata ndiyo msingi wa mafanikio yao katika matumizi ya mikopo na kwamba ni wajibu wa kila mshiriki kuhakikisha fedha wanazokopeshwa zinatumika kwa uadilifu ili biashara zao ziwe endelevu.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Bi Nyamayao Said, jumla ya washiriki zaidi ya 400 wameshiriki katika mafunzo hayo. Hawa ni kutoka makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambao wote wamekidhi masharti ya kupata mikopo kutoka halmashauri. Bi Nyamayao alieleza kuwa mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi muhimu kabla ya utoaji rasmi wa mikopo hiyo.


Aidha, Bi Nyamayao alibainisha kuwa mbali na elimu ya ujasiriamali, washiriki pia watafundishwa mbinu za kujenga nidhamu ya kifedha, namna ya kutunza kumbukumbu za biashara na namna ya kujenga mitandao ya masoko kwa bidhaa au huduma watakazozalisha. Mafunzo hayo yatachukua muda wa siku kadhaa kabla ya zoezi la utoaji wa mikopo kuanza rasmi.


Mkurugenzi Possi amewahakikishia washiriki kuwa halmashauri itaendelea kuwa bega kwa bega nao hata baada ya mikopo kutolewa kwa kuhakikisha wanapata ushauri wa kitaalamu na ufuatiliaji wa maendeleo ya miradi yao. Ameeleza kuwa dhamira ya halmashauri ni kuona wananchi wake wanainuka kiuchumi kupitia mpango huu.


Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za serikali za kuwainua wananchi kiuchumi kupitia uwezeshaji wa moja kwa moja kwa makundi maalum, na yanatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya washiriki na jamii zao kwa ujumla. Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze inatarajia kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa mpango huu wa kitaifa wa utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze afungua mafunzo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu

    September 26, 2025
  • Maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima yafanyika Chalinze

    September 03, 2025
  • Tume ya Utumishi wa Umma Kufanya Ukaguzi Chalinze

    September 01, 2025
  • Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata yafunguliwa Rasmi

    August 04, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.