Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani hii leo wamemthibitisha Mhe. Hassan Mwinyikondo diwani wa Kata ya Msoga kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze akichukua nafasi ya Mhe Godfrey Kamugisha.
Zoezi hilo lilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chalinze ambapo madiwani walipiga kura za ndio au hapana kwa jina moja lililopitishwa na chama ambapo Mhe. Mwinyikondo alipigiwa kura zote za madiwani waliokuwepo na kuapishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mhe.Hashim na baadae kamati ya Uchumi na Mazingira imemchagua Mh.Malota Kwaga Diwani wa kata ya Kiwangwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi na Mazingira ili kujaza nafasi ya mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Shariff Zahoro amempongeza Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Chalinze kwa kuchaguliwa kuiongoza Halmashauri hiyo na kuwataka Waheshimiwa madiwani na Watendaji kutoa ushirikiano.
Nikupongeze kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti na niwapongeze madiwani wote waliokuchagua wewe na inaonesha mna ushirikiano mzuri kwani wamekupigia kura zote lakini pia ninaomba nikupe nasaha zangu kwako ni kusimama imara kwa kuhakikisha Halmashauri inakwenda kwa kasi kubwa sana kwani Chama ,Madiwani na Watendaji wana imani na wewe na ukafanye kazi kwa kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili Chalinze iende mbele vilevile niwaombe Waheshimiwa Madiwani na Watendaji mumpe ushirikiano,na ushauri mzuri Mwenyekiti wetu mpya lakini pia kuwepo na mshikamano madhubuti ili jahazi la Halmashauri ya Chalinze linafika salama”.Alisema Mhe.Shariff.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zaibabu Abdallah amempogeza Mhe. Mwinyikondo kwa kupewa dhamana ya kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na kumshauri Mwenyekiti mpya wa Halmashauri mambo matatu muhimu yatakayosaidia kuiongoza vyema Halmashauri ikiwemo mapato na matumizi,kusimamia miradi na Kuwa kiunganishi.
“ Nichukue fursa hii kwaniaba ya ofisi ya Wilaya kumpongeza Mhe. Mwinyikondo kwa kuchaguliwa na Chama kwa kura nyingi na kuthibitishwa na Madiwani kwa kishindo na hii inaonesha Waheshimiwa madiwani wana imani na wewe lakini pia binafsi nimeona kazi kubwa unayoifanya na katika ushauri wangu Mhe. Mwenyekiti ninaomba uzingatie mambo haya matatu ikiwemo usimamizi wa mapato na matumizi ikiwa huu ndio msingi mkuu wa Halmashauri na ikizingatiwa kwa mwaka huu tumepanga kukusanya Bilioni 10.7 hivyo niombe hakikisha tunakusanya mapato na tunavuka malengo, pia tunamshkuru mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za UVIKO-19 zaidi ya Bilioni moja kwaajili ya ujenzi wa madarasa hivyo basi ukasimamie miradi hii kwa nguvu zako zote na kwakuwa umeapishwa na kuthibitishwa leo tunaomba tuungane mimi pamoja na kamati ya usalama kukagua miradi hiyo ya madarasa kuona miradi hiyo inaendelea vyema na kuona thamani ya ujenzi inakidhi ili kufikia tarehe 30/12/2021 miradi hiyo iwe imekamilika kama ilivyoelekezwa na TAMISEMI, jambo la pili ni kusimamia vyema miradi ya huduma za jamii ili kuona fedha inatumika kwa usahihi na pia usimamie miradi yote ikiwemo TFS,DAWASA,RUWASA na TANESCO na jambo la tatu ni kuwa kiunganishi kati ya Halamshauri na Chama Cha Chapinduzi,halmashauri na serikali kuu kwa kushirikina na kuwa kiunganishi kati yako Mwenyekiti na Halmashauri kwa maana ya madiwani wote wa Chalinze” Alisema Mhe. Zainab Abdallah.
“Lakini pia niwashukuru Waheshimiwa Madiwani kwa kupitia Mwenge wa Uhuru Wilaya yetu imepata bahati ya kuwa wa kwanza Kimkoa,watatu kikanda na wa sita Kitaifa na hiyo yote ni ushirikiano wa Madiwani mpaka kufika hapa, hivyo kwaniaba ya Serikali ninawashukuru sana kwa ushirikiano katika kuweka heshima kubwa kimkoa na nina imani kwa mwaka ujao tutajitahidi ili ikimpendeza Mungu tuwe wa Kwanza Kitaifa.” Aliongeza Mhe. Zainabu Abdallah.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe. Hassan Mwinyikondo ametoa neno la Shukrani kwa Chama Chama Cha Mapinduzi,Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Madiwani wote kwa dhamana aliyopewa
Kutoka ndani ya moyo wangu ninashukuru Chama Cha Mapinduzi CCM, Mkuu wa Wilaya Pamoja na Madiwani kwa dhamana kubwa sana mliyonipa ya kuisimamia Halmashauri ya Chalinze na ninawaahidi sitowaangusha na ninapenda kusema Uchaguzi umekwisha hivyo basi sisi madiwani wote tuungane na tushirikiane kuhakikisha Halmashauri inakwenda kwani tumepokea nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali na kwa Chama chetu cha Mapinduzi CCM na kwa Mkuu wa Wilaya na ninahakikisha nasaha hizo tunazifuata
114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.