• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Ridhiwani:Umiliki wa Ardhi Kisheria Suluhisho la Migogoro Nchini

Imewekwa: March 8th, 2022

NAIBU Waziri Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amesema ili kuondokana na migogoro ya ardhi ni vema kila mwananchi ahakikishe ana hati miliki ya eneo lake.



Ridhiwani aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Kwamsanja, Kwamduma na Kwakonje ambapo wananchi walimuelezea kuhusiana na migogoro isiyoisha inayosababisha kutokuwa na maendeleo.



Alisema kero ya migogoro ya ardhi imekuwa ikielezewa na wananchi katika maeneo mbalimbali aliyopita na muarobaini wa tatizo hilo ni kuwa na hati miliki ambayo itakuwa inaelezea mipaka ya kila mmoja pamoja na vijiji.



"Wenyeviti hakikisheni wananchi wanapimiwa maeneo wanakuwa na hati miliki ili kuondoa hii migogoro ya mara kwa mara, simamieni pia vijini vyenu vihakikiwe mipaka yake itasaidia kufanya shughuli nyingine za maendeleo badala ya kila siku kufanya usuluhishi" alisema.



Kuhusiana na suala la mifugo kuharibu mazao ya wakulima Rishiwani aliwataka watendaji kusimamia sheria ndogo zinazotungwa na baraza la Madiwani ili kukomesha hali hiyo.



Ofisa  Ardhi wa Halmashauri ya Chalinze Musa Kichumu aliahidi kushughulikia maagizo ya Naibu Waziri huyo huku akiwataka wananchi kuheshimu mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao kila mmoja ametengewa eneo lake kwa jamii ya wafugaji na wakulima.



Aidha alieleza kuwa  kuwa ipo haja ya elimu kwa wananchi kuhusiana na mpango wa matumizi bora ya ardhi ili wasisitizwe kuzingatia mipango hiyo kuepuka migogoro ya mara kwa mara.



Ofisa Mifugo wa Halmashauri ya Chalinze Msongo Songoro alisema kuwa ipo sheria imepitishwa na Madiwani ambayo inasubiri Waziri wa Tamisemi kusaini na itakapoanza kila ng'ombe atakayekutwa kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kisheria atatozwa sh.50,000 kwa kila ng'ombe mmoja.



Songoro alisema sheria  hiyo ni kati ya zilizotungwa na Halmashauri kuondoa migoro kwenye baadhi ya maeneo ya Halmashauri hiyo  mingi ikihusishwa wafugaji wanaolalamikiwa kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima.



Ofisa Mifugo huyo pia aliwataka wazazi kuwalea watoto wao kwa kufuata maadili ili kuepuka kushiriki kwenye wizi wa mifugo ambao nao unaelezwa kutokea kwenye vijiji huku wanaotajwa kuhusika wakiwa ni Vijana.



 Wakizungumza katika mikutano tofauti iliyofanywa na Naibu Waziri  huyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, walimueleza kuwa wanashindwa kufanya shughuli za kimaendeleo kutokana muda mwingi kutumia wakisuluhisha migogoro.



Ramadhani Mtui na Juma Chambila wakazi wa Kibindu walieleza kuwa kwenye baadhi ya mashamba yao wanashindwa kuendesha shughuli za kilimo kutokana na jamii ya wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba yao.



Mtui aliiomba Serikali kuingilia kati kwani kuna hatari ya kukumbwa na baa la njaa kwa jamii ya wakulima endapo hakutakuwa na udibiti wa mifugo kwenye maeneo ya kilimo.



Katika kijiji cha Kwakonje wananchi waliomba kuwepo kwa kituo cha polisi kudhibiti matukio yanayodaiwa kufanywa na jamii ya wafugaji ambao wanashindwa kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.