• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wajumbe wa mabaraza ya Kata Chalinze wapata mafunzo

Imewekwa: November 12th, 2018




Kitengo cha Sheria katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze kimetoa mafunzo ya kuyajengea uwezo mabaraza ya kata tisa kati ya kumi na tano kuhusu sheria  na taratibu  zinazoongoza mabaraza ya kata kwa mujibu wa sheria ya Mabaraza ya kata namba 7 ya mwaka 1985.

Mafunzo hayo yametolewa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 kwa wajumbe wapatao 72 na watendaji wa kata 9. Kata zilizopata mafunzo hayo ni kata za Msata,Mandera,Kiwangwa,Miono,Msoga,Lugoba,Bwilingu,Pera na Vigwaza.


     Mafunzo hayo ni kwa ajili ya wajumbe wote wa mabaraza la kata pamoja na watendaji wa kata ili kuwajengea uwezo wajumbe wote pamoja na watendaji juu ya sheria,taratibu na miongozo mbalimbali inayotumika katika kuyaongoza mabaraza ya kata. Kwa mujibu wa Mwanasheria wa halmashauri Bi. Happyphania Luena, alitoa ufafanuzi kwa kueleza walichojifunza wajumbe wa mabaraza ya kata ni pamoja na maana ya mabaraza ya kata,sheria za mabaraza ya kata,mabaraza ya kata na mashauri ya ardhi,muundo wa mabaraza hayo,namna wanavyopatikana wajumbe na sifa zao,ukomo na mamlaka ya baraza la kata  na rufaa na marejeo dhidi ya maamuzi ya baraza la kata


.Mwanasheria wa halmashauri alifafanua kwa kueleza kuwa ,lengo la halmashauri ni kutoa mafunzo kwa mabaraza yote ya kata na kwa kata sita zilizobaki watapata mafunzo kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2018/2019


   Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze, Saidi Zikatimu akizungumza na waandishi wa tovuti ya halmashauri kuhusu mafunzo ya kuwawezesha wajumbe wa mabaraza ya kata aliipongeza ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia kitengo cha sheria kwa hatua za makusudi walizochukua kutoa elimu ya namna ya kuendesha mabaraza hayo,na kusema kuwa kuyawezesha mabaraza ya kata ni chanzo cha kuondoa migogoro mbalimbali ya ardhi na kutolewa ufumbuzi usiokuwa na mashaka kwa kutoa uamuzi au hukumu stahiki kwa wananchi wanaobishania juu ya haki zao, utatolewa kwa misingi ya sheria taratibu na kanuni kwa kuzingatia sheria ya mabaraza ya kata na si vinginevyo.


   Aidha Mheshimiwa Zikatimu aliendelea kufafanua kuwa endapo mabaraza hayo yatafanya kazi kwa umakini na weledi yatapunguza msongamano wa mashauri katika Baraza la ardhi na nyumba wilaya kwani rufaa zinaweza kupungua kama siyo kwisha kabisa."Elimu hii kama itatumika ipasavyo itakuwa msaada hata kwa mabaraza ya ardhi ya vijiji katika utoaji hukumu na maamuzi mbalimbali na itapendeza Elimu hii ikitolewa hata katika halmashauri za vijiji kwa halmashauri ya Chalinze ili kuboresha utawala wa sheria."Zikatimu alisema.





Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.