• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Walimu wa kike wa Shule za Sekondari 22 wapewa mafunzo ya stadi za maisha na elimu ya fedha

Imewekwa: March 10th, 2022

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ikishirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la “Room to read” hii leo imeanza mafunzo maalumu ya stadi za maisha na elimu ya fedha kwa walimu wa kike katika shule 22 za sekondari ikiwa kila shule imetoa mwalimu mmoja wa kike kama mwakilishi wa shule yake.

Mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ni miongoni mwa mradi mkubwa unaofanywa na shirika la “Room to Read” ambao unaitwa mradi wa nguvu ya msichana  ukiwa na lengo la kuwapa mafunzo ya stadi za maisha na elimu ya fedha walimu wa kike wa shule za sekondari zilizopo katika Halmashauri hii na kwenda kuyatumia kuwezesha wanafunzi waliopo katika shule zao.

Akizungumzia malengo ya mradi huu mratibu wa mafunzo hayo ndugu Abdourlahman Banza amesema mradi wa nguvu ya msichana ni mradi ulio na mafanikio makubwa hasa kwa Halmashuri ya Wilaya Chalinze na umelenga katika kuwafanya wasichana wa shule za sekondari waweze kubaki shuleni na kupata stadi za msingi za kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao ya sasa na ya Baadaye.

“Mradi wetu wa nguvu ya msichana ambao umejikita katika kutoa mafunzo kuhusu stadi za maisha na elimu ya fedha kwa msichana na kijana aliyepo shuleni umelenga kumsaidia kijana na mtoto wa kike kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maisha yake ya kawaida na kupata kizazi kinachoweza kujitetea, pia kumwezesha binti kujidhibiti na kufanya matumizi mazuri ya fedha pamoja na kuweza kujua misingi ya ujasiriamali na  Biashara.”Alisema Ndg. Abdourlahman Banza

Aidha Afisa mradi Bi Rehema Juakali aliongeza kwa kusema kuwa mradi huu ni ushirikiano baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze pamoja na shirika la ‘Room to read’ umelenga kuwatumia walimu ili kuweza kuwafikishia wanafunzi waliopo katika shule zao.

“Mradi huu unaofanyika hapa Chalinze, unalenga kuwapa mafunzo walimu wawakilishi wa shule 22 ambao watapewa mafunzo na kuweza kuyafikisha nakuyawezesha kwa wanafunzi waliopo katika shule zao wanazofundisha ili elimu ya stadi za maisha na elimu ya fedha iweze kuwafikia wasichana wengi waliopo shuleni na vijana kwa ujumla”.Alisema Bi. Rehema.

Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo Mwl. Husna Luvanga ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Kikaro ameelezea namna mafunzo yanavyoendelea na jinsi gani anaamini mafunzo hayo yatawasaidia wanafunzi wa kikenaweza kutumia mafunzo aliyoyapata ili kuweza kuwawezesha wanafunzi wake elimu wanayoendelea kuipata.

“ Tunashukuru mafunzo yameanza vizuri na kiukweli mafunzo haya tunayopewa na wawezeshaji wetu ni mazuri na nina Imani tutakapowafikishia wananfunzi wetu wataelewa na kuyatumia vyema na pia naamini mpaka mwisho wa mafunzo haya tutakuwa tumepata kitu kikubwa kikubwa sana” Alisema Mwl.Husna.

Mafunzo hayo ya siku 6 ni matokeo ya ushirikiano na makubaliano baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze pamoja na taasisi ya ‘Room to read’ ambapo yatawezesha kuibadilisha jamii hasa wasichana.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.