• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wataalamu wa Wizara ya Ardhi,Halmashauri na Asasi zisizo za kiserikali watoa mafunzo kwa kamati ya urasimishaji ardhi kitongoji cha Pera

Imewekwa: July 19th, 2023


Wataalamu kutoka wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,wataalamu wa halmashauri na Asasi za kiraia wamefika katika kitongoji cha Pera katika kata ya Pera  ili kuhamasisha na kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya Mradi wa Uboreshaji usalama wa Milki za Ardhi (Land Tenure Improvement Project). Mradi huu ni mradi unaotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze.


Wataalamu hao wamefika katika kitongoji hicho ili kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hiyo sanjari na kufahamu majukumu yao kama wajumbe wa kuwaunganisha wananchi na wataalamu watakaokuwa wakishughulika na kazi ya kupima na kurahisisha zoezi la urasimishaji. Akifafanua majukumu ya wanakamati Afisa Mipango Miji wa Halmashauri Bi Rogate Johnson aliwaeleza wajumbe hao majukumu yao ni pamoja na kuandaa mikutano ya wananchi,kuelimisha umma na kutatua migohoro kwa maeneo yatakayokuwa na migogoro katika zoezi la urasimishaji.


Bi Rogate Johnson aliongezea kuwa wanakamati ni kiunganishi na chachu ya kufanikisha zoezi hilo na kuwaeleza kuwa wajumbe wa kamati hii watashiriki katika zoezi la upimaji kuanzia mwanzo wa zoezi hadi mwisho sanjari na kuwandaa wananchi kwa zoezi la upimaji na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu.


Akitoa ufafanuzi zaidi Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Chalinze Bwana Deo Msilu aliwataka wanakamati kuwa wahamasishaji wakuu katika zoezi hili ili kurahisisha kazi na kukamilisha kwa wakati ili kufikia malengo ya serikali kupima viwanja zaidi ya elfu kumi katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze.


Naye Mwakilishi wa Wizara ya Ardhi Bi. Judith Lugeye aliwataka wanakamati kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya utaifa kwa kila mwananchi ili kurahisisha zoezi katika umilki wa ardhi kwa mujibu wa sheria. Sanjari na hilo aliwataka wananchi kusajili ardhi zao kwa pamoja kwa wanandoa kama watakuwa tayari kumilki ardhi yao kwa pamoja,hata wale wenye ndoa za mitala wanaruhusiwa kumilki ardhi kwa pamoja pasipo shaka sheria inaruhusu.


Naye mwakilishi kutoka asasi za kiraia Bwana John Batoga aliwataka wakamati wa kamati ya urasimishaji kuzingatia sheria taratibu na kanuni ili kuzingatia haki za binadamu kwa kuzingatia makundi maalumu katika zoezi hili kama walemavu ,wazee wasiojiweza,wagonjwa wa muda mrefu, watoto yatima na wajane ambao wana nyumba au ardhi yao ili kuepuka wajanja wachache kujimilikisha ili hali ardhi siyo mali yao. Aliwaasa kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kulinda haki za binadamu kwa wananchi wote.


Mwakilishi wa asasi za kiraia aliwataka wanakamati kuwashirikisha wanawake katika zoezi hili kwani nao wanahaki ya kumilki ardhi kama wanaume sanjari na vijana wa kike na kiume nao wanayohaki ya kushiriki katika zoezi hili.


Kwa Upande wake Afisa Mazingira wa halmashauri ya Chalinze Bwana Aswile Mwangobola aliwataka wanakamati wa kamati ya urasimishaji kuzingatia sheria za mazingira katika suala zima la urasimishaji kwa kulinda mabonde na vyanzo vya maji pasipo kuviathiri au kuleta madhara kwa wananchi wengine kama mafuriko pale inapotokea ujenzi umefanyika na kuzuia njia za maji.


Afisa Maendeleo ya Jamii,Bi Spora Elisante aliwataka wanakamati kutumia lugha nzuri na yenye hamasa kwa wananchi ili kuepuka migogoro ambayo inaweza kutokana na lugha zisizo kuwa na staha,hali kadhalika alitoa tahadhari kwa wanakamati kutoa elimu ya mapambano dhidi ya magonjwa kama Ukimwi kwa wananchi sambamba na kutoa tahadhari kwa vijana wetu wa kike kujiepusha na madhara yanayoweza kutokea kutokana na mwingiliano wa watu wengi katika mradi huu wa urasimishaji. Sanjari na kuepuka vijana wetu kupata ujauzito usiokuwa na walezi au baba wa watoto watakaozaliwa pasipo utaratibu na kuleta athari katika jamii.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.