• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Watumiaji wa umeme watakiwa kufanya maboresho ya LUKU kwa matumizi sahihi

Imewekwa: July 23rd, 2024

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kanda ya Mashariki limewataka watumiaji wa mfumo wa lipa umeme kadiri unavyotumia(LUKU) kushiriki kufanya maboresho yanayoendelea kwenye mfumo huo ili kuendelea kupata huduma hiyo.

Hayo yamesemwa na  Afisa mahusiano na wateja wilaya  Charles Vincent leo Julai 22,2024 alipokuwa akifanya mahojiano na  kituo cha Chalinze fm kwenye kipindi cha Gumzo leo kinachoruka kila jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 04:00 hadi saa 07:00 mchana.

Aidha maboresho hayo kwa Mkoa wa Pwani yameanza leo Julai 22, yenye lengo la kufanya maboresho ili kuendana na viwango vya Kimataifa na kuongeza ufanisi Zaidi  na usalama wa mita hizo nchini Tanzania.

Afisa mahusiano Vincent akieleza namna mteja atakapo nunua umeme atapokea tarakimu 60 kwenye makundi matatu, na kusema kuwa kila kundi litakuwa na tarakimu 20.Aidha makundi mawili ya kwanza  yatakuwa kwaajili ya maboresho na kundi moja la mwisho litakuwa  la umeme alionunua  hivyo  mteja  anapaswa kuingiza  tarakimu za kila kundi kwa mfuatano unaosomeka kwenye risiti ya malipo au ujumbe mfupi wa simu alio pokea mara baada ya kununa umeme huo ,na kila atakapo ingiza kundi moja mteja atapwa kuponyeza alama ya okey/kukubali na hapo atakuwa amefanikiwa kuboresha mita yake na atapokea kiwango cha umeme alicho nunua.

Sanjari na hayo Vincent ametoa  angalizo kwa baadhi ya  wateja wanaonunua umeme na kuuhifadhi wanapaswa kuweka umeme huo kwenye mita zao kabla ya kununua umeme mpya na zoezi hilo mteja hatotozwa gharama yoyote.

Kwa upande wake Mdhibiti wa mapato ya umeme kutoka shirika la umeme Tanesco Ibrahim Mkumbukwa amesema kwa mteja mita yake itakayo kataa kupokea mabadiliko anapaswa kutoa taarifa kupitia namba  0748 550 000 za huduma kwa mteja  ili aweze kupata msaada,na  kwa wateja wa mkoa wa Pwani wataweza kupata huduma kupitia namba 0738 256237.Pia ametaja mita namba zitakazo fanyiwa maboresho ili kuendana na mfumo mpya ni zile zinazo anza na 24210, 0134, 075 na 04.

Ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zoezi hili linatarajiwa kutamatika ifikapo Novemba 24 ,2024 kwa mikoa yote nchini.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.