• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

Imewekwa: July 9th, 2025


Na John Mlyambate

CHALINZE, PWANI — Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya chanjo ya mifugo leo tarehe 9 Julai 2025 katika kijiji cha Kikaro, Kata ya Miono, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani.


Uzinduzi huu ni muendelezo wa kampeni iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyefungua rasmi zoezi hilo kitaifa katika mji wa Bariadi, Mkoa wa Simiyu, kwa lengo la kuboresha afya ya mifugo nchini.


Waziri Kijaji ameambatana na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani, pamoja na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, ambao wataendesha zoezi hilo kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe ya uzinduzi.


Katika hotuba yake, Dkt. Kijaji alieleza kuwa kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wa kuboresha sekta ya mifugo kwa kutoa chanjo bora kwa wanyama ili kuongeza thamani na ushindani wa mifugo ya Tanzania katika soko la ndani na la kimataifa.


Alisisitiza kuwa kuchanja mifugo ni hatua muhimu kwa wafugaji kwani husaidia kupunguza vifo vya mifugo, kuboresha afya yake, na kufungua milango ya biashara katika masoko ya nje ambako usalama wa chakula ni kipimo kikuu cha ubora wa bidhaa.


Aidha, Waziri Kijaji aliwahamasisha wafugaji wote kote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la chanjo ili kunufaika na faida mbalimbali za kiuchumi na kiafya zinazotokana na mifugo iliyopewa chanjo sahihi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mheshimiwa Shaibu Ndemanga, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alitoa shukrani kwa serikali kwa hatua hiyo muhimu ya kutoa chanjo kwa mifugo yote ikiwemo kuku, mbuzi, kondoo na ng’ombe, akisema hatua hiyo itachangia kukuza soko la nyama.


Mheshimiwa Ndemanga alisema serikali inatekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuinua maisha ya wafugaji kwa kuwasaidia kuongeza kipato kupitia uwekezaji kwenye sekta ya mifugo kwa kutoa huduma za chanjo na usajili wa mifugo kwa kipindi hiki cha kampeni.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Pwani, Bwana Rashidi Ngobele, alitoa shukrani kwa niaba ya wafugaji wote kwa serikali kwa kuboresha huduma za mifugo na kuonyesha dhamira ya kweli ya kulinda rasilimali hiyo muhimu kwa uchumi wa wafugaji na taifa kwa ujumla.


Alitoa wito kwa wafugaji wote nchini kuitikia wito wa kampeni hiyo kwa ari na mshikamano, akisisitiza kuwa zoezi hilo lina faida kwa vizazi vya sasa na vijavyo kwa kuwa linajenga msingi imara wa ustawi wa sekta ya mifugo nchini.


Zoezi la utoaji wa chanjo litaendelea katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha siku 30, ambapo timu za wataalamu zitatoa huduma ya chanjo na elimu kwa wafugaji ili kuhakikisha ufanisi na uelewa mpana wa zoezi hili la kitaifa.


Kampeni hii inatarajiwa kuwafikia maelfu ya wafugaji na mifugo katika mikoa yote ya Tanzania, ikiwa ni jitihada mahsusi za serikali katika kulinda afya ya mifugo na kukuza pato la taifa kupitia sekta ya mifugo yenye ushindani wa kimataifa.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

    July 09, 2025
  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.