• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Ziara ya ukaguzi wa maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Chalinze

Imewekwa: September 20th, 2019

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Serikari za Mitaa  Halmashuri ya Wilaya ya Chalinze Ndg. Shabani Millao akiambatana na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Ndg. Lington Zambi wamefanya ziara katika kijiji cha Mindutulieni kilichopo katika Kata ya Lugoba na kijiji cha  Diozile kilichopo katika Kata ya Msoga siku ya Alhamisi (Jana)  kwa Lengo la Kukagua maendeleo ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kukuta baadhi ya malalamiko kutoka kwa wananchi wa Mindutulieni wakidai kubandikwa kwa baadhi ya Matangazo ya majina na mipaka ya vijiji na vitongoji linalohusu Kata ya Msoga hasa  Diozile kubandikwa katika eneo la Mindutulieni.
‘’Tunashangaa kuona Tangazo la Uchaguzi linalohusu kijiji cha Diozile kubandikwa katika maeneo yetu hii inaashiria wanataka mgogoro nasi ambapo sisi hatutaki litokee jambo hilo.’’ Alisema mzee Ikoyo Mtumia mkazi wa kijiji cha Mindutulieni.’’
Nae Mtendaji wa kijiji cha Mindutulieni Ndg. Godfrey Nyange amethibitisha uwepo wa Matangazo hayo yaliyobandikwa katika kijiji chao na kusababisha taharuki kwa wananchi wa kijiji hicho na kwa kufanya hivyo ni kitu ambacho kinaashiria uchokozi wa makusudi kwakuwa eneo hilo bado lina Mgogoro wa mipaka.
Kwa upande wa Mtendaji wa kijiji cha Diozile Bi.Mariam Mkombezi Bakari ameshangazwa na hatua hiyo ya wananchi wa kijiji chake kwa kusema.
‘’Nashangazwa na habari hii ya kuwekwa kwa baadhi ya matangazo ya Kijiji chetu katika kijiji jirani cha Mindutulieni na hawa watu ni watu wenye nia mbaya ya uchochezi baina ya vijiji vyetu ambapo si jambo zuri hata kidogo.’’
Msimamizi mkuu wa Uchaguzi wa Wilaya ya Chalinze  Ndg Shabani Milao ametoa tamko kwa Vijiji  hivyo viwili (Mindutulieni na Dihozile) Mara baada ya kupokea malalamiko hayo na kujionea tukio hilo hivyo akatoa tamko…
‘’Naomba niseme kwamba zoezi la Uchaguzi litaendelea kama lilivyopangwa katika mpangilio mzima wa upigaji kura kama ilivyoelekezwa na Serikali katika Matangazo yake, Hivyo naomba Uchaguzi huu uwe wa amani na utulivu katika vijiji vyote na ninyi watendaji wa Vijiji ndio muwe viongozi wa kuchochea  amani kwa wananchi wenu na mripoti matukio yoyote yanayoashiria uvunjifu wa amani katika Uchaguzi  ili kuwachukulia hatua wanaohusika.’’.Milao alisema.
Aliongeza kwa kusema..
‘’Navisihi vijiji vingine ambavyo vina migogoro ya mipaka visihusishe migogoro hiyo na uchaguzi kwani ni vitu viwili tofauti na kwamba suala la migogoro ya mipaka itatatuliwa kupitia ngazi husika hata baada ya uchaguzi hivyo kwa sasa tuangalie suala la Uchaguzi ili tupate Viongozi Imara kwa ajili ya Maendeleo ya Vijiji vyetu na jamii kwa ujumla.’’
Ikumbukwe kuwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika Novemba 24, 2019 Hivyo kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajitahidi kufanya jitihada katika maandalizi ya Uchaguzi huo ili Uchaguzi huo kuwa wa haki na wa amani.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.