IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII
Idara ya maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii ni moja ya kati ya idara 13 zilizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.
Jukumu kubwa la Idara ni kuiwezesha Jamii kuweza kutambua mahitaji na matatizo yake yenyewe na kuchukua hatua za kubaini ufumbuzi wa matatizo au mahitaji yake kwa kutumia rasilimali zilizopo ndani na nje
MUUNDO WA IDARA
Idara ya maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii imegawanyika katika vitengo 7 ambavyo hufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanapatikana, vitengo hivyo ni pamoja na:-
1. Mipango utafiti na Takwimu
2. Maendeleo ya wanawake na Dawati la jinsia
3. Maendeleo ya vijana
4. Ustawi wa jamii na watoto
5. Ukimwi
6. Uratibu wa Asasi zisizo za kiserikali(NGOs)
7. Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi
MAJUKUMU YA VITENGO NDANI YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
1. MIPANGO UTAFITI NA TAKWIMU
2. MAENDELEO YA WANAWAKE NA DAWATI LA JINSIA
3. MAENDELEO YA VIJANA
4.USTAWI WA JAMII NA WATOTO
5. UKIMWI
6. URATIBU WA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI (NGOs)
7. DAWATI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
i. Kusimamia na kufuatilia shughuli za uwezeshaji zinazofanywa katika kata na vijiji/mitaa katika Halmashauri
ii. Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika Halmashauri
iii. Kukusanya taarifa na tafi ti mbalimbali na kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri katika masuala ya uwezeshaji kiuchumi
iv. Kuhakikisha fedha za uendeshaji zinatengwa katika bajeti kila mwaka kwa ajili ya masuala ya uwezeshaji
v. Kuhakikisha kuwa Halmashauri inahusisha suala la hifadhi ya Mazingira na mabadiliko ya Tabia Nchi katika Mipango ya Maendeleo ya Wilaya ili kuboresha mazingira ambayo ni muhimu katika suala zima la uzalishaji mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
vi. Kubuni na kutafuta vyanzo vya rasilimali kwa ajili ya shughuli za uwezeshaji katika Halmashauri yake
vii. Kuratibu na kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa vikundi vya kiuchumi kama SACCOS, VICOBA na vingine vinavyosajiliwa na kutambuliwa toka ngazi ya wilaya hadi taifa
viii. Kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Kamati ya Uwezeshaji ya Halmashauri na baada ya kuidhinishwa itumwe kwa Mratibu wa Uwezeshaji Mkoa na nakala kwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
ix. Kuhamasisha vikundi vya kijamii na kiuchumi kujisajili/kujirasimisha na kufanya uzalishaji wenye viwango vya TBS, TFDA na kupata nembo ya utambuzi wa bidhaa (msimbomilia (Barcode))
x. Kuandaa taarifa ya maendeleo ya vyama vya ushirika hasa SACCOS na vikundi vya kiuchumi kama VICOBA vilivyopo katika Halmashauri
xi. Kubuni fursa mbalimbali za uwekezaji katika Halmashauri; xii. Kufuatilia upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kiuchumi
xii. Kushauri namna ya uboreshaji wa vituo vidogovidogo vya kibiashara, hususan, katika vijiji na Mamlaka za Miji Midogo.
Katika kukabiliana na changamoto za utandawazi na mabadiliko ya mila na desturi, maisha ya mwanadamu na Jamii kwa ujumla yamekuwa yakikabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Hivyo njia pekee ya kukabiliana na changamoto hizi ni kuhakikisha Jamii inashirikishwa ipasavyo katika kukabiliana na utatuzi wa changamoto zake zenyewe. Katika hili Idara ya Maendelea ya Jamii na Usatawi wa Jamii ni daraja muhimu.
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.