• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

Imewekwa: June 18th, 2025


Na Johnn Mlyambate

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bwana Rashid Mchatta, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa kupata hati safi mfululizo kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2023/2024. Pongezi hizo zilitolewa leo, wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Chalinze.


Katika hotuba yake, Bwana Mchatta alieleza kuwa hati hizo safi ni ushahidi wa usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mujibu wa bajeti na sheria, sambamba na juhudi kubwa zinazofanywa na viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo. Alibainisha kuwa licha ya mafanikio hayo, bado kuna hoja tisa za ukaguzi ambazo hazijafungwa, nyingi zikiwa ni za kisera.


“Ni jambo la kujivunia kuona hoja zimepungua kutoka 25 hadi 9, lakini halmashauri bado inapaswa kuhakikisha haina hoja yoyote inayozalishwa upya kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha na mifumo ya TEHAMA,” alisema Bwana Mchatta.


Aidha, alitoa maelekezo mahsusi kuwa ifikapo Septemba 30, 2025, hoja zote zilizosalia ziwe zimejibiwa na kufungwa kikamilifu.


Kwa upande wake, Bwana Pastori Masawe, Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Pwani, aliipongeza halmashauri kwa kujibu hoja kwa usahihi na kufanikisha kufungwa kwake, huku akihimiza kuendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya matumizi ya fedha ili kuepusha hoja mpya.


Pongezi zaidi zilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mheshimiwa Shaibu Ndemanga, aliyesifu usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha na kuzingatia sheria na taratibu za fedha, huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Bwana Abubakar Mlawa, akilitumia jukwaa hilo kuwapongeza madiwani na wataalamu kwa ushirikiano na utekelezaji madhubuti wa majukumu yao.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mheshimiwa Hasani Mwinyikondo, alipokea pongezi hizo kwa niaba ya halmashauri na kutumia fursa hiyo kuaga kwa niaba ya madiwani, akiwashukuru watendaji wote kwa ushirikiano waliouonesha katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wao.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Kampeni ya Ugawaji vyandarua bila malipo yazinduliwa Chalinze

    July 10, 2025
  • Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

    July 09, 2025
  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.