• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

Imewekwa: June 13th, 2025


Na John Mlyambate

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mheshimiwa Mary Pius Chatanda, amefanya ziara ya kikazi wilayani Chalinze, mkoani Pwani, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, hususan katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo.


Ziara hiyo ilifanyika tarehe 12 Juni 2025, ambapo Mheshimiwa Chatanda aliambatana na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya UWT Taifa, Mheshimiwa Subira Mgalu, na walipokelewa na mwenyeji wao, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Mheshimiwa Abubakar Mlawa. Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea utekelezaji wa miradi ya serikali na kushuhudia namna wanawake wanavyonufaika na fursa za kiuchumi kupitia mikopo na shughuli za uzalishaji.


Akiwa wilayani Chalinze, Mheshimiwa Chatanda alikagua ujenzi wa nyumba za wakuu wa Idara na Vitengo, ambazo zimejengwa kwa fedha kutoka serikali kuu. Alieleza kuridhishwa na hatua ya ujenzi na kupongeza watendaji wa serikali kwa kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa mradi huo ambao umelenga kupunguza changamoto ya makazi kwa watumishi wa umma.


Katika hatua nyingine, alitembelea mradi wa wanawake wa kufyatua matofali ulioanzishwa na kikundi kilichopata mkopo kutoka halmashauri ya Chalinze kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani. Aliwapongeza wanawake hao kwa mshikamano na ubunifu wao katika kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli hiyo ya uzalishaji wa vifaa vya ujenzi.


Mheshimiwa Chatanda alitumia fursa hiyo kumwomba Mkuu wa Wilaya ya Chalinze kuwapatia kikundi hicho fursa ya kuuza matofali yao kwenye miradi ya serikali inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo, ili kuongeza kipato na kukuza mtaji wao kwa maendeleo endelevu.


Aidha, katika sekta ya elimu, alitembelea Shule ya Sekondari ya Jakaya Mrisho Kikwete na kukagua miundombinu ya shule hiyo, ikiwemo mabweni, madarasa na nyumba za walimu. Alizungumza na wanafunzi pamoja na walimu kujua changamoto zinazowakabili, na kuahidi kuzifikisha katika mamlaka husika ili zipatiwe ufumbuzi.


Katika sekta ya afya, Chatanda alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Msoga na kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la utawala linaloendelea kujengwa kwa fedha kutoka serikali kuu. Alieleza kuridhishwa na kasi na ubora wa kazi inayoendelea kufanyika kwenye hospitali hiyo muhimu kwa wananchi wa Chalinze.


Akihitimisha ziara hiyo, Mheshimiwa Chatanda alisisitiza umuhimu wa uzalendo na uadilifu kwa wataalamu wote wa halmashauri katika kusimamia miradi ya maendeleo. Alisema mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM yanatokana na usimamizi mzuri wa miradi, hivyo ni muhimu kuendeleza juhudi hizo kwa manufaa ya wananchi wote.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • DC Ndemanga Aongoza Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe

    June 10, 2025
  • Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Tukamisasa waazimia Mwenyekiti Kupisha Uchunguzi

    June 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.