Majukumu ya Idara ya Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ni kama yafuatayo
• Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu katika mfumo rasmi na Elimu nje ya mfumo rasmi katika Halmashauri.
• Kuandikisha watoto wa darasa la kwanza wenye umri wa miaka ya kwenda shule.
• Kuelimisha jamii kushiriki katika mambo mbali mbali ya shule kupitia vikao vya mitaa ambavyo wananchi watahudhuria na kutoa maoni.
• Kuandaa bajeti ya idara na vitengo vyake ikiwa ni pamoja na mpango kazi unaoendana na bajeti hiyo.
• Kusimamia na kuendeleza taaluma katika Halmashauri ya Mtwara kwa kusimamia ufundishaji, ujifunzaji mahudhurio ya walimu, wanafunzi na utendaji kazi kwa ujumla.
• Kuandaa takwimu mbalimbali za kielimu za wanafunzi, walimu, samani na miundombinu.
• Kuratibu mashindano ya ya taaluma na michezo kwa shule za msingi.
• Kusimamia haki na maslahi ya walimu kwa kufuata taratibu kama vile ruhusa, likizo masomo, matibabu n.k.
• Kuhudumia jamii kuhusiana na mambo yote ya kielimu na mafunzo mbalimbali kupitia kamati za shule na shuguli nyinginezo kama vile uhamisho wa wanafunzi.
• Kuandaa na kuendesha vikao mbalimbali vya wadau wa elimu katika ngazi zote za Halmashauri.
• Kuandaa Tange ya walimu wa shule za msingi kwa kila mwaka
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.