Majukumu ya Idara ya Elimu Sekondari katika Halmashauri
• Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu shughuli zote zinazohusu Idara ya Elimu ya Sekondari
• Kusimamia mitihani yote ya ndani na ile ya Taifa yaani Mitihani ya kidato cha II,IV, VI na Vyuo vya Ualimu
• Kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli za ujenzi wa miundombinu katika shule za Sekondari kama vile nyumba za walimu, madarasa, majengo ya utawala, maabara, mkataba na vyoo
• Kusimamia na kuratibu shughuli zote za Ukusanyaji, uchambuzi na kutafsiri takwimu za Idara ya elimu Sekondari na kuzituma kwa wadau wa elimu
• Kusimamia na kuratibu shughuli za uandaaji wa taarifa na kuzituma kwa wadau mbalimbali wa elimu ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa
• Kusimamia na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata taaluma kwa kiwango kilicho bora kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 na 2014.
• Kusimamia na kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi, walimu na watumishi wasio walimu inadumishwa shuleni
• Kusimamia na kuhakikisha fedha za Idara ya Elimu Sekondari zinatumika kwa kufuata kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya fedha za Serekali za Mitaa
• Kuhakikisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinapatikana katika shule za sekondari
• Kuhakikisha kuwa shule zote za Sekondari zina samani za kutosha kwa ajili ya walimu na wanafunzi
• Kuandaa ajenda na kuhudhuria vikao vyote vinavyohusu Idara ya Elimu Sekondari
• Kuandaa taarifa za utekelezaji za Idara ya elimu sekondari za robo na mwaka na kuziwasilisha kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile Waheshimiwa Madiwani, Mkoa na Taifa
• Kuandaa makisio ya bajeti ya Idara ya Elimu ya Sekondari kila mwaka.
• Kupokea na kuwapangia vituo walimu na wafanyakazi wa idara wanaohamia au wanaoajiriwa katika Halmashauri
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +25523233456
Simu ya mkononi: +255766050788
Barua pepe : ded.chalinze@pwani.go.tz
Haki Miliki @2017 Halmashauri yaWilaya ya Chalinze .Haki zote zimehifadhiwa