Ukweli kuhusu hifadhi ya Taifa ya Saadani:
Ukweli namba moja ni kuwa Saadani ni Hifadhi ya Taifa inayopatikana katika Halmashauri ya Chalinze na ni Hifadhi iliyoko karibu kabisa na Jiji la Dar es Salaam takribani ni Umbali wa Km 130 tu. Hifadhi hii iko mkabala na Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Hifadhi ya Taifa pekee nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki yenye fukwe za bahari na inayotazamana na Bahari ya Hindi. Ni hifadhi pekee ambapo fukwe za bahari zake zinakutana na uoto wa asili wa nchi kavu.
Uwepo wa hifadhi ya Taifa ya Saadani ni matokeo ya pori la akiba la Saadani, ranchi ya mkwaja na sehemu ya Kaskazini ya mkwaja sambamba na akiba ya msitu wa asili wa Zaraninge. Hifadhi hii inapatikana baina ya Mkoa wa Tanga na Pwani.
MAANDALIZI YA USAFIRI:
Ni pamoja na kufahamu gharama za jumla za safari yenu ya matembezi hifadhini Saadani.
Ufahamu wa maandalizi haya yazingatie mambo muhimu ya Kimsingi kama vile Usafiri, Sehemu za huduma za chakula, malazi au kulala na mengineyo yatakayojitokeza .
Baada ya haya yote kutekelezwa kwa ukamilifu na umakini mkubwa kitakachofuatilia ni mpango mkakati wa fedha za maandalizi zilizopatikana. Mwisho kabisa ni bajeti ya fedha za maandalizi kuandaliwa jinsi zilivyopangiliwa.
KUANZISHWA KWAKE:
Ilianzishwa mwaka 2005. Tangu miaka ya 1960, eneo hili la Saadani ilikuwa ni moja ya maeneo ya pori la akiba la wanyamapori.
ENEO LAKE:
Ukubwa wa eneo la hifadhi ya Taifa ya Saadani ni ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 1,178. Nchi kavu inachukua ukubwa wa kilomita za mraba 1,148 na kilomita za mraba 30 ni eneo la maji ya bahari ya hindi.
UFIKAJI HIFADHINI;
Hifadhi ya Taifa ya Saadani inafikika umbali wa kilomita 50 kutoka visiwa vya Zanzibari na inachukua saa 3 kwa njia ya usafiri wa majini wa kutumia ngalawa na vile vile ni dakika takribani 50 kwa njia ya usafiri wa majini wa kutumia boti. Vile vile ni sawa na kilomita 45 kutoka mji wa kihistoria wa Bagamoyo.( dakika 40) na Dar es salaam ni kilomita 100.
MAUMBILE ASILIA YA KIJIOGRAFIA HIFADHINI:
Tambarare za pwani, vilima vidogo vidogo, mlima kiono unaohifadhi msitu wa asili wa zaraninge kwa upande wa kusini Magharibi.
Upande wa Kaskazini wa Mkwaja una mandhari nzuri yenye kupendeza ya makazi ya vilima vya hapa na pale. Kwa upande wa kusini ni Bonde la mto Wami.
HALI YA HEWA USAWA WA BAHARI HIFADHINI:
Inaanzia 0 mpaka 350 kutoka usawa wa bahari.
VIVUTIO VIKUU VYA UTALII HIFADHINI:
Fukwe na Bahari, kasa wenye viota vya mayai ardhini katika eneo la madete. Vile vile mto wami una aina mbalimbali za wanyamapori na ndege, mikoko pamoja na maji ya bahari yanayokutana na mto (Estuaries).
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.