UTANGULIZI
Serikali imekuwa ikitoa maelekezo ya namna ya kushugulikia malalamiko katika Taasisi za zake ikiwa ni pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Maelekezo hayo yamekuwa yakitolewa kwa njia ya mafunzo na nyaraka mbalimabli. Kipeperushi hiki kimetumia maelezo yaliyotolewa na Ofisi ya Rais Ikulu katika kikao cha kazi kwa Wakuu wa Idara ya Utawala na Utumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wataalam wa Sekretarieti za Mikoa kilichofanyika tarehe 14 -19 Desemba, 2009.
1.0 MAANA YA MALALAMIKO:
Malalamiko yanaweza kutafsiriwa kama maelezo au tamko la kuonyesha kutoridhika kuhusu jambo lolote. Kutoridhika huko kunaweza kuwa ni kuhusu uamuzi au utekelezaji wa suala fulani. Malalamiko yanaweza kusababisha ufanisi na ushirikiano hasa mahala pa kazi ukapungua hivyo kuleta athari za kiutendaji kazi.
1.2 WAKATI GANI MTEJA KATIKA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA ANAWEZA KUTOA MALALAMIKO:
Mteja katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa anaweza kutoa malalamiko yake pale ambapo ataona uamuzi ama utekelezaji wa jambo fulani siyo sahihi, siyo wa haki au ni kinyume cha Sheria na taratibu zilizowekwa.
1.3 UMUHIMU WA KUSIKILIZA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO:
Kusikiliza na kushughulikia malalamiko mahali popote ni muhimu kwasababu:
Ni njia mojawapo ya kutumikia jamii na kutatua matatizo ya watumishi.
Inasaidia kuwepo amani na utulivu katika jamii na mahala pa kazi.
Inasaida kuwepo na ushirikiano mahala pa kazi hivyo kuleta utendaji mzuri mahala pa kazi.
Ni njia nzuri ya kuelewa matatizo yanayowakabili watu.
Vilevile inasaidia kuelewa kama kuna dosari katika mfumo wa uendeshaji au udhaifu wa watendaji wenyewe.
Hivyo, ni lazima kila mtendaji kwenye nafasi yake awajibike ipasavyo kuhakikisha malalamiko yanapungua. Haimaanishi kupunguza malalamiko kwa kuwakataa walalamikaji bali kwa kufanya yafautayo:-
Kuzingatia Sheria na Taratibu wakati wote wa utendaji wa kazi.
Kuwajibika na kutekeleza majukumu ipasavyo na kwa wakati muafaka.
Kutenda haki kwa kila mtu wakati wote.
Kuepuka upendeleo.
Kutotenda uonevu..
2.0 UTARATIBU WA KUSHUGHUKILIA MALALAMIKO.
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM TAMISEMI) inapokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mikoa na wananchi wa kawaida kuhusu masuala mbalimbali ambayo pengine yanahusiana na huduma wanazopaswa kupata toka Halmashauri, Mikoa, Ofisi nyingine za Serikali.
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.