• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DC Bagamoyo awataka wananchi kuheshimu mipaka ya vijiji kuepuka migogoro

Imewekwa: September 25th, 2019


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Zainabu Kawawa amewataka wananchi wa vijiji vya Chamakweza na Pingo katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze kuheshimu mipaka ya vijiji vyao na kuacha tabia ya kuuza ardhi kiholela pasipo kuzingatia sheria taratibu na kanuni za ardhi.


Kawawa ameyasema hayo katika mikutano ya kusikiliza kero na migogoro ya ardhi kwa wananchi wa vijiji vya Chamakweza na Pingo jana,katika mikutano yake hiyo wananchi walitoa malalamiko yao kwa kueleza kuwa mipaka ya vijiji hivyo ina utata unaosababisha baadhi ya wananchi kuuza ardhi ya upande wa kijiji jirani bila kujiridhisha kama eneo linalouzwa liko katika kijiji cha mtu anayeuza hivyo kusababisha mtafaruku baina  ya pande mbili za vijiji jirani.


Mkuu wa wilaya katika kutafuta ukweli wa malalamiko ya pande zote mbili alifanya mkutano katika kijiji cha Chamakweza na kusikiliza malalamiko ya wananchi hao ndipo alienda hadi eneo linalosemekana kuuzwa kiholela, na baada ya hapo alienda moja kwa moja katika kijiji cha Pingo na kufanya mkutano na wananchi pia alisikiliza malalamiko yao dhidi ya upande wa pili.


Kawawa baada ya kupata malalamiko ya wananchi wa vijiji hivyo alitaka maelezo kutoka ofisi ya ardhi wilaya kuhusu malalamiko ya wananchi hao kuhusu mpaka wa vijiji hivyo.

Mtaalamu wa upimaji ardhi Jackson Mchomvu alibainisha mipaka ya vijiji hivyo ambavyo vilipimwa na wataalam wa wizara ya ardhi tangu mwaka 2010,mpaka halisi unaotenganisha hivi vijiji kutoka kusini hadi kaskazini ni kutoka mto Msua hadi mto Mbiki,ndio mpaka unaotambulika kwa sasa ambapo awali mto Mbiki ndio uliotenganisha vijiji vya Talawanda na Chamakweza kwa upande wa Mashariki na Pingo kwa upande wa Magharibi.


  Kwa mujibu wa mtaalam huyo eneo kutoka Mto Mbiki hadi Mto Mpapaya ni eneo ambalo lilikuwa halijapata muafaka kuwa ni la upande wa Chamakweza au Pingo. Mwaka 2014 wataalam kutoka wizara ya ardhi walifika ili kukaa na wananchi kuhusu eneo ambalo halikupata muafaka wananchi wa pande zote mbili hawakuweza kukubaliana hivyo muafaka haukupatikana.”Kimsingi eneo hili ndiyo chanzo cha migogoro na mwingiliano wa wananchi katika matumizi ya ardhi hii”. Mchomvu alisema.


Baada ya ufafanuzi uliotolewa na Mpima Ardhi wa halmashauri na kupata uhalisia wa mipaka ya kila kijiji,Mkuu wa wilaya alitoa maagizo kwa kwa wananchi wa vijiji vyote viwili kuheshimu mipaka hiyo na kuheshimu matumizi ya ardhi kutokana na mpango wa matumizi sahihi ya ardhi,viongozi kuheshimu sheria ya ardhi kwa kuepuka uuzaji wa ardhi ya kijiji kiholela ili kuepuka migogoro ya ardhi inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.


Aidha Mheshimiwa Kawawa aliendelea kusema,kwa kipande cha ardhi ambacho bado hakijafikiwa muafaka na vijiji vyote viwili yaani kutoka mto Mbiki hadi Mpapaya kitapatiwa muafaka na wananchi wa pande zote mbili.” Hivyo wananchi wa Chamakweza na Pingo wataalam wa wizara ya ardhi watafika kuiweka sawa mipaka yenu toeni ushirikiano kwa wataalam hao ili mufikie makubaliano yenye tija na yenye kutatua migogoro kwa pande zote mbili.” Mkuu wa wilaya alisisitiza.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.