• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Elimu Bila Malipo si Kigezo cha Kukwepa Majukumu-Samataba

Imewekwa: July 10th, 2018

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani,Zuberi Samataba amekemea upotoshaji wa dhana ya Elimu bure unaopelekea wananchi wa mkoa wa Pwani kurudisha nyuma ufanisi wa kiutendaji katika sekta ya Elimu, kauli hiyo ameitoa hivi karibuni katika maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Chalinze.Kutokana na upotoshaji huu wazazi na wanajamii waliowengi wanaona kuwa hawana wajibu wowote ule katika kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu katika shule zetu wakiami kuwa hiyo ni kazi ya serikali.”Tafsiri hii si sahihi na ni kikwazo katika kutekeleza dhamira ya elimu bila malipo kwenye maeneo yetu”.Samataba alisema.

Katibu Tawala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alifafanua zaidi wakati wa hotuba yake kwa kusema ,Waraka wa Elimu Na.6 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Elimu bila malipo umebainisha wazi majukumu ya kila mdau wa elimu kama vile serikali,wazazi,walezi,walimu,kamati na bodi za shule na jamii kwa ujumla.

Samataba alisisitiza kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu inayosema”Uwajibikaji wa Pamoja kwa Elimu Bora kwa wote”kutokana na kaulimbiu hii ni wazi kabisa kuwa kama kila mdau atawajibika kwa kutekeleza yanayotakiwa kwa mujibu wa waraka namba 6 wa elimu bila malipo wa mwaka 2015,adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bila malipo kwa watanzania itatekelezeka kwa vitendo.

Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Pwani Bi Hilderguard Makundi aliishukuru serikali ya awamu ya tano kutokana na mpango wa elimu bila malipo kwani kiasi cha uandikishaji kwa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza kimepanda kwa kuvuka lengo kwa mwaka 2018  ambapo tulitarajia kuandikisha wanafunzi 47,686 lakini tumeandikisha wanafunzi 52,551 sawa na asilimia 110  haya yote ni matokeo ya mpango huu wa elimu bila malipo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani,Mheshimiwa Ramadhani Maneno alitoa neno la shukrani kwa serikali ya awamu ya tano kwa jinsi inavyotekeleza mpango wa elimu bila malipo kwa mkoa wa Pwani na matokeo ya mpango huu,aidha aliishukuru serikali ya mkoa kwa usimamizi bora wa mipango ya serikali na kuwataka waendelee kuwa na moyo katika kuwatumikia watanzania wa mkoa wa Pwani na hata baada ya kuwa wametoka katika mkoa huu nyayo zao zikaonekane kutokana na utendaji wao.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.