• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Elimu ya Lishe bora kwa vitendo yafika kata ya Mbwewe.

Imewekwa: October 28th, 2021

Idara ya Afya kitengo cha lishe bora Halmashauri ya Wilaya ya chalinze imeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu ya uaandaji na matumizi ya lishe bora kwa kundi la kina mama wenye watoto chini ya miaka 5 na wajawazito katika kata ya Mbwewe ikiwa ni moja ya sehemu ya kuimarisha afya bora kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.

Akizungumza kwa niaba ya mganga Mkuu wa Wilaya, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bi. Zainabu Waziri ameelezea dhumuni la kutoa elimu hiyo ni kuwaelimisha akina mama juu ya umuhimu wa lishe bora KWA WATOTO WAO.

“tumekuja kata ya Mbwewe kutoa elimu hii ya lishe bora kwa vitendo ikiwa ni jinsi ya kuandaa na faida za lishe bora kwa watoto walio chini ya miaka mitano na mama wajawazito kulingana na mahitaji ya vyakula ambavyo vipo katika jamii zao na hiyo itasaidia kupunguza tatizo la utapiamlo kwa watoto hasa kwenye kata hii na hatutaishia hapa tutafika mpaka ngazi za vijiji ili kuendelea kutoa elimu hii”.Alisema Bi.Zainabu Waziri.

Hata hivyo afisa lishe huyo amevitaja vyakula ambavyo vikichanganywa vinaunda lishe bora ikiwa ni pamoja na unga wa dona, maziwa,karoti, ubuyu, mafuta ya kula na sukari na amesisitiza kuwa hakuna chakula ambacho kina virutubisho vyote Zaidi ya maziwa ya mama pekee.

Aidha kwaniaba ya wahudumu wa afya ya msingi jamii, Bi. Pilly Mbwana ameahidi kuendeleza na kudumisha zoezi la elimu ya lishe bora ili liwe endelevu.

“ Kwanza tunashukuru kwa muitikio huu wa leo kwani hii itasaidia kuwapasha habari wale wachache ambao hawakufika siku hii ya leo kuapata elimu hii muhimu na sisi kama wahudumu wa afya ya msingi jamii tutajitahidi kuendeleza mafunzo tuliyoyapata siku ya leo”. Alisema Bi.Pilly Mbwana.

Nae Bi. Fatma Haji mkazi wa Mbwewe ambae ni miongoni mwa mama aliyepata elimu hiyo ya lishe bora ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa jitihada zake za kuimarisha afya ya mama na mtoto na kuiomba Halmashauri kuendeleza elimu hiyo.

“ Napenda kuishukuru Halmashauri yetu ya Chalinze kwa jitihada zake mpaka kupata mafunzo haya ya lishe bora kwa vitendo kwani tunaweza kuitumia elimu hii tuliyopata kuimarisha afya za watoto wetu na pia niiombe Halmashauri isiishie hapa bali iendelea kutoa elimu ya lishe bora kwenye vijiji vyetu”. Alisema Bi. Fatma Haji

Utoaji wa Elimu ya lishe bora kwa vitendo ni mundelezo wa kampeni iliyowekwa na Idara ya Afya kitengo cha Lishe bora Halmashauri ya Chalinze ambapo imeandaa utoaji wa elimu hiyo katika vijiji 10 ndani ya Kata 3 ikiwemo Kata ya Mandera, Mbwewe na Kibindu.


Picha ya pamoja ya Afisa Lishe na wahudumu wa Afya ya Msingi jamii.


Wahudhuriaji wa elimu ya lishe bora kwa vitendo kata ya Mbwewe wakipewa elimu.


Maandalizi ya Uji wa Lishe bora.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.