• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Chalinze,Wadau wa Maendeleo wajadili matumizi na mpangilio bora kituo Kipya cha Mabasi Chalinze.

Imewekwa: October 7th, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze hii leo imefanya kikao na wadau wa maendeleo hususani madereva, makondakta, wafanyabiashara, mama lishe, Bodaboda na wengineo kwa lengo la kujadili ni kwa namna gani kituo kipya cha mabasi kitakuwa katika mpangilio mzuri na matumizi sahihi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Afisa Mipango wa Halmashauri Ndg. Shabani Millao amewaalika wadau hao ili kutoa maoni yao kuhusu namna bora ya uendeshaji wa kituo kipya cha mabasi mpangilio mzuri uliowekwa na kuzingatia usafi.

“Kwa naiaba ya Mkurugenzi wetu Ndg. Ramdhani Possi tumewaalika hapa wadau wakubwa wa maendeleo ya  Halmashauri yetu hususani watu mnao jishughurisha na kazi mbalimbali  katika kituo cha mabasi, ambao mnategemea kufanya kazi kwenye kituo chetu kipya cha mabasi tunachotarajia kukifungua siku chache zijazo, lengo kuu likiwa ni kuwashirikisha kutoa maoni yenu namna gani tunaweza kuweka mpangilio mizuri wa matumizi ya kituo chetu kipya kwani ninyi ndio wadau wakubwa wa sehemu hiyo”.Alisema Ndg. Shabani Millao.

Nao baadhi ya wadau waliipongeza Halmashauri ya Chalinze kwa hatua na jitihada zinazofanywa na Halmashauri hiyo za kushirikisha wadau na wananchi ili kuongeza ufanisi na ushirikiano katika kuletea maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.

“ Kwanza nipende kuipongeza Halmashauri yetu kwa hatua kubwa wanayofanya ya kutushirikisha kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanisi na ushirikiano ili kuleta maendeleo, pia niiombe Halmashauri iendelee kushirikisha wadau katika miradi mbalimbali ijayo”.Alisema Ndg. Shomari Lugazo.

Aidha katika kikao hicho Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Chalinze Dkt. Allen Mlekwa aliwaasa wananchi na wadau hao kuendelea kujikinga na ugonjwa hatari wa UVIKO-19 wawapo katika shughuli zao na familia zao pia.

“ Niwashukuru kwa kufika kwenu katika kikao hiki cha kimaendeleo lakini pia nipende kuwakumbusha kuendelea kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa pamoja na pata chanjo kwani chanjo hizo zinatolewa bure na zinapatikana katika vituo vyetu vya Afya. Alisema Dkt. Allen Mlekwa.   

Kikao hicho ni muendeleo wa vikao shirikishi vinavyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa kujumuisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kutoa maoni yao kuhusu shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Baadhi ya Wadau wa Maendeleo wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi standi ya 

mabasi Chalize wakiwa katika kikao cha kujadili namna Bora ya uendeshaji wa kituo

kipya cha mabasi Chalinze.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata yafunguliwa Rasmi

    August 04, 2025
  • Maandalizi ya Maonyesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yapamba moto

    July 29, 2025
  • Halmashauri ya wilaya ya Chalinze kujenga kituo cha mafuta kwa mapato ya ndani

    July 16, 2025
  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze Atembelea maonyesho ya 49 ya Saba saba

    July 14, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.