• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya upimaji ardhi Chalinze kutaongeza kasi ya Upimaji wa Viwanja kutoka wastani wa viwanja vitano (5) kwa siku hadi viwanja 200 kwa siku

Imewekwa: March 3rd, 2021

Halmashauri ya Chalinze, imepokea Vifaa  vipya vya kisasa vya kupima Ardhi ili kuwezesha upimaji wa Viwanja na kupanga mji wa Chalinze kwa kasi.

Tukio hilo la makabidhiano lifanyika jana Tarehe 2.02.2021 baina ya viongozi wa kampuni ya  Global Survey na viongozi mbalimbali wa Halmashuri katika viwanja vya Makao makuu ya Halmashauri ya Chalinze wakiongozwa na  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nfugu: Ramadhani Possi, Mwenyekiti wa Halmashauri Geofrey Kamugisha, Mbunge wa jimbo Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete pamoja na baadhi ya Madiwani walioonesha furaha yao katika kuona Ardhi inakwenda kupimwa hali itakayoongeza thamani yake.

Awali akizungumza wakati wa kuvipokea vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ndugu. Ramadhani Possi alisema vitawasadia kama watendaji kwendana na kasi ya upimaji wa Ardhi ambayo walitarajia na vinaenda kutumika kupima ardhi yote ilikuendelea kuvutia Waekezaji na kutatua migogoro yote ya ardhi inayoikumba Halmashauri ya Chalinze

"Lengo la Halmashauri yetu ni kuendelea kuvutia uwekezaji na moja ya vigezo ni kuwa na ardhi iliyopimwa ili kuwahakikishia Wawekezji watakaokuja kwenye Halmashauri uhalari wa umiliki wa Ardhi kwa ajili ya uwekezaji kwenye Viwanda, Hotel, Vituo vya Afya, Yumba za kulala wageni na maeneo mengine ya uwekezaji.Kupitia vifaa hivi tutaendelea kupima viwanja vya makazi, viwanja vya biashara, pamoja na vya viwanda." Alisema Ndugu. Ramdhani Possi.

Aidha, aliongeza kuwa, kama watendaji kupitia idara ya ardhi tumejipanga  kwenda kupima viwanja kwa kasi ya ajabu kwa kutumia vifaa hivyo vya kisasa kwa lengo la kuongeza pato la Halmashauri kwa kupitia chanzo hicho cha mapato.

"Tuliadhimia ili twende na  kasi ya upimaji wa ardhi kwa haraka, Kama Halmashauri tumenunua kifaa hiki Cha kisasa aina ya RTK ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa katika moja ya vikao vyetu na Waheshimiwa Madiwani na sasa tunaona mwanga mzuri wa Chalinze iliopangika, Maana huwezi kupima viwanja vingi bila kuwa na vifaa bora na vya kisasa." Alisema Ndugu, Ramadhani Possi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Geofrey Kamugisha alishukuru kampuni la Global Survey kwa kuleta vifaa hivyo kwa wakati na uongozi wa Chalinze chini ya Mkurugenzi mtendaji  Ndugu: Ramadhani Possi kwa ununuzi wa Vifaa hivyo na kwamba utaleta ukombozi mpya kwa Chalinze katika swala la upimaji wa ardhi

Kumekuwa na kusuasua kwa upimaji wa viwanja katika Halmashauri yetu kwa muda mrefu ujio wa vifaa hivi ni ukombozi wa tatizo hili na tunategemea kuiona Chalinze mpya Chalinze iliopangika. Wito wangu kwenu wataalamu wa ardhi mliopo Halmshauri mkiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu. Ramadhani Possi ni kuvitumia vifaa hivi tulivyokabidhiwa leo kwa lengo kusudiwa pia ni sharti tuvitunze ili viweze kudumu kwa Muda mrefu na kuleta manufaa kwa jamii nzima ya Chalinze.  Alisema Mh. Geofrey Kamugisha

Nae Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh, Ridhiwani Kikwete  alishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kutekeleza maagizo yaliotolewa na Baraza la Madiwani na maagizo ya Viongozi wa juu wa Halmashauri

"Mashine hii  ya kupima na kupanga ardhi imekuja wakati mwafaka, Zamani Wapima wetu waliweza kupima na kuchora viwanja Vitano (5) hadi Kumi (10) kwa Siku.

Ujio wake itawezesha Halmashauri kupima viwanja 150 hadi 200 kwa Siku sawa na viwanja 1000 kwa Wiki." Alisema Ridhiwani Kikwete.

Ni imani yangu kuwa katika zoezi la upimaji ardhi litakalo fanyika Halmashauri ya Chalinze, maeneo ya taasisi za serikali ikiwemo Shule za Msingi na Sekondari, Zahanati, Vituo vya Afya na Zahanati vitapewa kipaombele ili kuweza kutatua migogoro inayoendelea baina ya wananchi na taasii hizo. Aliongeza Mh. Ridhiwani Kikwete

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa kampuni ya Global Survey, Abdul Mlanzi  alibainisha kuwa, kifaa hiko kinachofahamika kama Real Time Kainematik (RTK) ni cha kisasa ambapo kina  uwezo wa kupima viwanja kuanzia hadi 100 hadi 200 kwa siku.

"Kampuni yetu pia ipo tayari  kuendesha mafunzo maalum ya jinsi ya kuvitumia vifaa hivi vya kisasa kwa watumishi wa idara ya ardhi wa Halmshauri. Vifaa hivi vipo katika mfumo wa kisasa ambapo duniani kote wanatumia hususani nchi zilizoendelea" alisema Abdul Mlanzi.

Wakichangia katika Hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo Kwa upande wao baadhi ya Madiwani walioshuhudia tukio hilo walibainisha kuwa, Chalinze inaenda kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi huku wakitarajia  kupanda kwa thamani kwa viwanja na ardhi  mara baada ya kuwa vimepimwa.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.