• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Ng’ombe wa maziwa atua kikundi cha Wanawake na maendeleo-Mazizi kata ya Msata

Imewekwa: October 10th, 2019

Kikundi cha Wanawake na Maendeleo-Mazizi kilichopo kijiji cha Mazizi kitongoji cha Mkwazu katika  kata ya Msata kimekabidhiwa Ng’ombe wa maziwa siku ya Jumatano ya tarehe 9/10/2019 ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Kopa ng’ombe lipa ng’ombe ulioanzishwa na Halmashauri  ya Wilaya ya Chalinze.

Ng’ombe huyo amekabidhiwa kwenye kikundi hicho na Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri Ndugu Hamza Chuguma pamoja na Afisa mifugo wa kata Bi.Agripina Silau mbele ya Diwani wa kata hiyo Mh.Selestine Semiono.

Mara baada ya makabidhiano hayo ndugu Chuguma amewasihi wanakikundi hao kuwa makini na ng’ombe huyo kwani kikundi hicho kina  bahati ya kupata ng’ombe huyo kwa awamu ya kwanza hivyo hawana budi kumtunza.

‘’Halmashauri ya Chalinze chini ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh.John Pombe Magufuli  imefanikiwa kutekeleza mradi huu kwa awamu ya kwanza katika kikundi chenu na kikubwa zaidi ngombe huyu ana mimba na anahitaji uangalizi hivyo hamna budi kumtunza ili kutaleta maendeleo kwenye kaya zenu na taifa kwa ujumla.’’ Alisema Ndugu Chuguma.

Nae Afisa ufugaji na uvuvi wa kata hiyo Bi. Agripine amekiambia kikundi hicho ataendelea kukipa mafunzo na njia mbalimbali ya jinsi gani ng’ombe huyo atatakiwa kutunzwa ili kutoa maziwa mengi kadri siku zitakavyokwenda. 

Aidha Diwani wa kata hiyo Mh.Semiono ameishukuru serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa kukiona kikundi hicho kukipatia Ng’ombe kupitia  mradi  wa Kopa ng’ombe lipa ng’ombe.

‘’Naishukuru sana  Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze iliyo chini ya Serikali yetu ya awamu ya tano kwa kufanikiwa utekelezaji wa mradi huu katika kikundi hiki cha kina mama ndani ya kata yetu naamini mradi huu ni chachu ya maendeleo kwa wananchi kuanzia mtu mmoja mmoja.’’ Alisema Mhe.Semiono

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi hicho Bi.Adela Joseph Zambeleti ameishukuru Halmashauri kwa kukipa kipaumbele kikundi chao katika mradi huo.

‘’Kwaniaba ya kikundi chetu cha Wanawake na Maendeleo –Mazizi tunasema ahsante kwa Halmashauri yetu ya Chalinze kwa kukiona kikundi chetu na kuwa moja ya vikundi vinavyopatiwa mradi huu hivyo tutahakikisha Ng’ombe huyu tuliopewa tunamtunza ili aweze kutuletea maendeleo katika kikundi na kata yetu.’’ Alisema Bi.Adela.

Na kwaniaba ya wanachi wa kitongoji cha Mkwazu wametoa shukrani zao kwa kuwakilishwa na Mwenyekiti wake Ndugu Mohamed Ally Masabwa kwa kusema.

‘’Shukrani kwa Serikali na Halmashauri yetu leo tumefurahi katika kitongoji chetu kwa kupata n’gombe huyu ambaye atatusaidia kupata maziwa kwajili ya matumizi ndani ya kijiji chetu na kujipatia kipato kwa kikundi cha kina mama hawa na kuweza kukuza maendeleo kwenye familia zao.’’

Ikumbukwe kuwa Mradi huu wa Kopa ng’ombe lipa ng’ombe ni endelevu kwani umetekelezwa kwa awamu ya kwanza kwa kununua ng’ombe 5 na kugawiwa kwa vikundi 5 katika kata 5 ikiwemo Kata ya Kiwangwa, Msata, Mboga, Msoga na Bwilingu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.