• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

RC Ndikilo afungua Miradi yenye thamani ya milioni 425.7 Chalinze

Imewekwa: February 27th, 2020


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,leo amekabidhiwa rasmi miradi ya sekta ya Elimu na Afya yenye jumla ya fedha za kitanzania milioni 425.7 na shirika la hifadhi ya taifa TANAPA.


Miradi aliyokabidhiwa ni nyumba ya mwalimu moja iliyojengwa katika shule ya msingi Saadani,kijiji cha Saadani,Kata ya Mkange, halmashauri ya Chalinze, yenye Thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya milioni 68.


Mradi mwingine ni Zahanati na vifaa tiba vyake na nyumba ya Mganga vyote vikiwa na Thamani ya fedha za kitanzania milioni 357.7, Zahanati hiyo imejengwa katika Kijiji Cha Mkange na Kata Mkange katika halmashauri ya Chalinze.


Taarifa ya kukabidhi Miradi hiyo ilitolewa kwa Mkuu wa Mkoa  na Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Mashariki Bi. Steria Ndaga ikifafanua namna TANAPA ilivyotekeleza jukumu la ujenzi wa Zahanati na nyumba za watumishi,kuwa ilikuwa ni hitaji la wananchi wa maeneo husika ambayo yaliibuliwa na kamati ya maendeleo ya Kata ya Mkange.


Bi.Ndaga katika taarifa yake aliwataka wananchi wanaozunguka hifadhi ya ya Saadani kuwa na ushirikiano na hifadhi ili kulinda wanyama na mazingira kwa ujumla,kwani kukiwa na uhusiano mzuri shirika litazalisha kwa tija na huduma za jamii zitaendelea kutokewa kutokana na faida ambayo shirika linapata." Pamoja na kukabidhi Miradi hii leo shirika limekuwa likijenga madarasa katika maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri ya Chalinze mfano, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kibindu." Ndaga alisema.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo,katika hotuba yake ya ufunguzi wa nyumba na Zahanati,alilipongeza shirika la TANAPA kwa juhudi linazoendelea kuzifanya katika kuboresha huduma za Afya kwa kujenga Zahanati nzuri na ya kisasa kwa wananchi wa Mkange,kitu ambacho lilikuwa ni hitaji la muda mrefu kwa wananchi hawa.


Mheshimiwa Ndikilo aliendelea kutoa wito kwa shirika la TANAPA kutochoka kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wote wanaozunguka hifadhi ya TANAPA Ili kutekeleza adhima ya serikali kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za Afya na Elimu bora kwa kila mtoto wa kitanzania.


Ndikilo aliwataka wananchi kuwa na uhusiano mzuri na hifadhi ya taifa,ikiwa ni pamoja na kuwalinda wanyama wetu,ambao kimsingi ndiyo waliotuletea leo Zahanati nzuri na nyumba za watumishi,hii ni kutokana na usimamizi bora wa shughuli za hifadhi unaopelekea shirika kupata faida na hatimaye faida hiyo kuwarudia wananchi kupitia huduma hizi za kijamii.


Naye Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete,katika neno lake la shukurani aliwapongeza na kuwashukuru shirika la TANAPA kwa kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo na kuwaomba waendelee zaidi na zaidi kuboresha mazingira ya wanachalinze katika nyanja mbalimbali za maisha hususan Elimu na Afya.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mheshimiwa Zainabu Rashidi Kawawa aliwataka wananchi waliokaribu na hifadhi ya taifa kupambana na vitendo viovu vinavyoweza kusababisha upotevu wa wanyama wetu katika hifadhi na pindi kunapokuwa na changamoto Kati ya hifadhi ya taifa na vijiji vinavyozunguka hifadhi hatua za haraka zichukuliwe ili kuboresha mahusiano mema kwa pande zote mbili.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.