Mbunge wa Viti maalum Mhe.Subira Mgalu amehimiza upendo na Uzalendo baina ya Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe. Hassan Mwinyikondo, Madiwani na Watendaji wa Halmashauri. Hayo Ameyasema leo katika baraza maalumu la madiwa la kumthibitisha na kumuapisha Mwenyekiti Alie Chaguliwa kwa ajili ya Kuchukua nafasi ya aliekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Geofrey Kamugisha
“Nikupongeze kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Halmashauri hivyo basi naomba utuunganishewote na kuimarisha ushirikiano na namuomba sana MwenyeziMungu atusimamie tutimize majukumu yetu na Niwaombe tupendane,tushirikiane na tutangulize uzalendo kwa rasilimali zinazopatikana Chalinze tuzisimamie vizuri na kutoa ushauri uliomzuri na yeyote anayetaka kututenganisha basi tumkemee ili Halmashauri yetu iweze kusonga mbele”. Alisema Mhe. Subira Mgalu
Aidha Mh. Mgalu alihitimisha kwa kuwataka Madiwani na wataalamu wote kuhakikisha wanaelekeza nguvu zao katika kuhakikisha wanaijenga Chalinze katika Misingi ya Maendeleo kwa kuwekeza zaidi katika Miradi Mikakati na kusimamia mapato na Matumizi kwa ustawi wa Chalinze
114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.