• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji waapishwa Chalinze

Imewekwa: November 30th, 2019


Kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 28/11/2019 leo wenyeviti wa vijiji ,vitongoji na wajumbe wa halmashauri za vijiji vilivyopo katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze wameapishwa rasmi katika ukumbi wa shule ya sekondari Lugoba ,hafla hiyo ya uapishwaji wa viongozi hao imehudhuriwa na wananchi mbalimbali kutoka maeneo wanakotoka viongozi hao.


Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Chalinze Bwana Shabani Millao amesema kwamba katika halmashauri yake viongozi wote walipita bila kupingwa kwa maana ya wenyeviti wa vijiji 74,wenyeviti wa vitongoji 469,wajumbe wa Halmashauri za vijiji 1318,hivyo kuleta jumla ya viongozi 1861 walioapishwa tayari kwa kuanza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na sheria ya serikali za mitaa ya namba 7 ya mwaka 1982.


Aidha katika zoezi la uapishaji yalitolewa mafunzo na miongozo ya namna ya uendeshaji wa serikali za vijiji na vitongoji kwa maana ya kuzingatia sheria taratibu na kanuni Za nchi bila kukiuka maadili ya uongozi katika jamii na wametakiwa viongozi hao kuwa chachu ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli yenye kauli mbiu isemayo “Hapa kazi tu”


Kwa upande wake Afisa TAKUKURU wa Chalinze Bwana Frank Duwe    

aliwaasa viongozi hao kupambana na vitendo vyote vinavyoashiria utoaji na upokeaji wa rushwa katika maeneo yao ya kazi na kuwa mabalozi wazuri wa mapambano dhidi ya rushwa katika Jamii.


Naye Afisa Usalama wilaya Bwana Ernest Singo Mbaya aliwataka viongozi hao kuwa walinzi wa amani na kuhakikisha wanazingatia viapo vyao kwa kuzisimamia sheria za nchi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na zaidi kutenda haki kwa wanaowaongoza katika maeneo yao ya utawala


Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Bi Jane Mfuko aliwataka viongozi hao kuzingatia utawala bora na shirikishi kwa kuwataka wawe na ushirikiano wa hali ya juu na watendaji wa vijiji na kata ili kuweza kutatua kero za wananchi katika maeneo yao ya utawala na hiyo mdiyo dhana ya utawala bora katika mamlaka za serikali za mitaa.”Msiwaachie watendaji peke yao katika maamuzi yanayohusu maslahi ya umma shirikianeni na mtoe maamuzi kwa pamoja”. Mfuko alisema.


Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Msoga,Mheshimiwa Imelda Raphael Ndaga aliwapa nasaha viongozi hao kabla ya kiapo na kuwataka waheshimu na kuzingatia maudhui ya kiapo na kufanya kazi ya kuhudumia wananchi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni za nchi.”Kiapo hiki ni kwa mujibu wa sheria hivyo mnatakiwa kuheshimu kiapo hiki muda wote wa uongozi wenu.”Hakimu alisema.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.