• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kata 12 kukaguliwa utekeleza wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Chalinze

Imewekwa: April 28th, 2018

Kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Bagamoyo imekagua jumla ya miradi ya maendeleo 20  katika kata 12 za halmashauri ya wilaya ya Chalinze hivi karibuni, miradi hiyo ni afya 10, elimu 5,viwanda 2,ofisi za watendaji 2 na soko 1,ikiwa ni moja ya kazi ya kamati hiyo kukagua na kuona utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya mwaka 2015-2020 inayotekelezwa kwa sasa nchini kote.

Katika ziara hiyo iliyolenga kufuatilia kwa kina utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM wajumbe walijikita zaidi katika kufuatilia ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii kwa maana ya afya, elimu,maji,nyumba za watumishi na kubaini ikama ya watumishi kwa kila kada.Hali kadhalika wajumbe wa kamati hiyo walitaka kufahamu namna ya utoaji huduma kwa wananchi katika maeneo waliyokagua ili kuona yaliyoahidiwa katika ilani kama yanatekelezeka kwa vitendo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Bwana Abdul-Rashid Zahor aliwataka wajumbe kukagua kwa kina na kubaini upungufu katika utekelezaji wa Ilani ya chama kwa mujibu wa ibara ya ya 49 hadi ya 58 inayo zungumzia sekta ya huduma za jamii.”Mwaka 2015 tuliahidi kwa wananchi kuboresha huduma za jamii kwa kuwahakikishia uwepo wa huduma bora za afya,elimu na maji,hivyo hatunabudi kuzisimamia halmashauri ili zitekeleze kwa wakati na bila kuchelewa kwani 2019 tutasimama kwa wananchi watatuhoji hivyo hatuko tayari kuhojiwa na kukosa majibu”Zahor alisema.

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo Bwana Kombo Kamote alifafanua kuwa katika ziara hii tulipanga kukagua miradi katika kata zote 15 za halmashauri ya Chalinze lakini hadi sasa tumeweza kuzifikia kata 12 na kutembelea miradi ya afya Lugoba,Msoga,Ubenazomozi,Mdaula,Chalinze,Buyuni,Changalikwa,Rupungwi,Kimange na Miono.Katika ziara hii tumebaini miradi ipo katika hatua mbalimbali ya ujenzi na inaendelea vizuri kwani mingine ni ya kumalizia na mingine bado iko katika hatua za msingi.Kwa upande wa sekta ya elimu tumekagua na kuona miradi katika shule za sekondari Chalinze,Changalikwa,Kimange,Kikaro na shule ya msingi Mbala.Katika elimu tumekagua ujenzi wa maabara,mabweni,nyumba za walimu,madarasa na bwalo,kwa upande wa viwanda tumeweza kukagua na kuona jinsi sekta binafsi zilivyolipokea tamko la serikali kuhusu viwanda kwa kuona uzalishaji katika kiwanda cha vigae kiitwacho “Twyford LTD”kilichopo katika kijiji cha Pingo kata ya Pera,kiwanda hiki kinazalisha vigae bora hapa nchini na kinauza vigae ndani na nje ya nchini kimeweza kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 900.Vilevile kamati ilitembelea kiwanda cha kuzalisha  vinywaji vinavyotokana na matunda mbalimbali kiitwacho” SAYONA FRUITS”kilichopo katika kijiji cha Msoga kata ya Msoga kiwanda hiki bado kinaendelea kujengwa na muda si mrefu kitaanza kufanya kazi na kitatoa ajira kwa wananchi.

                                                          Wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Bagamoyo wakikagua na kuona ujenzi wa kiwanda cha vinywaji cha "SAYONA FRUITS"kilichopo kata ya Msoga katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze

Aidha Kamote alibainisha changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa Ilani ikiwa ni pamoja na upungufu wa nyumba za watumishi wa sekta za afya na elimu,upungufu wa watumishi wa sekta hizi kwa upande wa elimu kuna upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati hii imedhihirika baada ya kamati ya siasa kutembelea shule ya sekondari ya Changalikwa ambayo ilibainika kuwa na mwalimu mmoja wa hisabati kwa shule nzima kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,Bwana Deogratius Lukomanya alizipokea changamoto zilizobainika katika ziara hiyo ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi zile zilizo ndani ya uwezo wa halmashauri na zile zinazohitaji utekelezaji wa serikali kuu kuzipeleka panapohusika kwa hatua zaidi.

Katika hitimisho wajumbe wa kamati ya siasa waliipongeza halmashauri kwa kutekeleza miradi mingi kwa kutumia mapato ya ndani ni uzalendo wa hali ya juu katika hili na wakaitaka halmashauri kuendelea kufanyakazi kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi ambayo ndiyo dira ya maendeleo kwa wanachalinze na watanzania kwa ujumla.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.